Makamu wa Rais ameahidi kuwapatia trekta
moja wakulima wa mkoa wa Mjini Magharibi ili liweze kusaidia wakulima kulima
kwa wakati.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati
alipotembelea Mradi wa Wakulima wa Mpunga katika bonde la Kizimbani lililobo
wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais aliwaambia wakulima hao kuwa Mjenga Nchi ni Mwanachi na aliwahimiza
viongozi wote kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za kuleta maendeleo na
kushirikiana bega kwa bega na wananchi.
Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya siku
nne ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ya CCM Zanzibar, amewataka viongozi na
wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi kushirikiana na kudumisha amani ya nchi.
Pamoja na kutembelea shamba la mpunga ambapo
alisimamia zoezi la upandaji mpunga Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea eneo
la Fuoni Kibaoni ambao alishuhudia upandwaji wa miti ya mikoko kwa kiasi
kikubwa ikiwa shemu ya utunzaji wa mazingira lakini pia utunzaji na uzalishaji
wa Kaa.
Katika ziara hiyo Makamu wa Rais aliambata
na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Mabodi, Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Magharibi Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja
na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.



0 Comments