Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiuliza swali la nyongeza kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba juu ya idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose
Tweve akiwa makini kuandika hoja ambazo anajibiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
Na Fredy Mgunda,Dodoma.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose
Tweve amelibana jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama
barabani kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na
hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo
Mbunge
Rose Tweve mapema hii leo bungeni aliuliza swali kwa wizara ya mambo ya
ndani ya nchi kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali
barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo.
Akijibu
swali la mbunge Rose Twelve Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mh. Mwigulu Nchemba alisema kuwa jeshi la polisi nchini kupitia kikosi
cha usalama barabani limeweza kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia
43 kwa mwaka 2017
Mwigulu
alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2017 kulitokea ajali 9856
ambazo zilisababisha vifo 3256 na majeruhi 2128 ambapo kwa mwaka 2017
kulitokea ajali 5310 na kusababisha vifo 2533 na majeruhi 5355.
Waziri
Mwigulu ameongeza kuwa kwa kipindi cha januari hadi februari 2018
kumetokea ajali 769 na kusababisha vifo 334 na majeruhi 698.
Akiuliza
swali la nyongeza mbunge Rose Tweve alimtaka waziri kutoa idadi ya
wahanga wa ajali waliolipwa fidia na mwaka 2009 bunge ilipitisha sheria
ndogo namba 10 ya bima ya kuwalinda wahanga wa ajali hizo,sasa mheshimu
waziri hawa wenzetu wa TIRA wanaonyesha wanamapungufu mengi na
watanzania wamekuwa wanahanga wakubwa kwenye swala hilo na kwanini
tusianzishe idara maalum ambayo itakuwa inatoa elimu kwa wahanga wa
ajali pindi inapotekea na kujua nini cha kufanya.
Akijibia
swali la Nyongeza la Mbunge Rose Tweve la kuhusu idadi ya wahanga wa
ajali waliolipwa fidia, Waziri Nchemba amebainisha kuwa katika kipindi
cha mwaka 2016-2018 jumla ya wahanga wa ajali 1583wakilipwa fidia takribani Bilioni 7 kutoka makampuni mbalimbali ya bima.
Katika
hatua nyingine Mwigulu Nchemba amekiri kuwepo kwa matukio ya ajali 1500
yanayosababishwa na uzembe wa madereva huku serikali ikipanga
kuwachukulia hatua madereva wenye tabia hizo.
“Ni
kweli serikali itahakikisha inawachukulia hatua madereva wazembe
ikiwemo kuwanyang’anya leseni ili kupunguza idadi ya madereva ambao
wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuepkukika” alisema Mwigulu
nchemba.


0 Comments