Afisa ardhi halmashauri ya Kibaha ,Frenk Mwalembe akiweka
X nyumba zilizo maeneo hatarishi nyakati za mvua katika kitongoji cha
Janga kata ya Janga ,ikiwa ni agizo la mkuu wa wilaya ya Kibaha
,Assumpter Mshama (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Moja ya nyumba zinazowekwa X maeneo hatarishi nyakati za mvua katika kitongoji cha Janga kata ya Janga ,ikiwa ni agizo la mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,katika zoezi hilo nyumba 50 zilizowekwa X na nyingine karibia 30 zipo ndani ya maji ambazo zitawekwa X .(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama (wa kushoto) akizungumza kwenye zoezi la kuweka X nyumba zilizo maeneo hatarishi nyakati za mvua katika kitongoji cha Janga kata ya Janga . (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Moja ya nyumba zinazowekwa X maeneo hatarishi nyakati za mvua katika kitongoji cha Janga kata ya Janga ,ikiwa ni agizo la mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,katika zoezi hilo nyumba 50 zilizowekwa X na nyingine karibia 30 zipo ndani ya maji ambazo zitawekwa X .(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama (wa kushoto) akizungumza kwenye zoezi la kuweka X nyumba zilizo maeneo hatarishi nyakati za mvua katika kitongoji cha Janga kata ya Janga . (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
SERIKALI
wilayani Kibaha ,Mkoani Pwani imeweka X katika nyumba karibia 80
,kitongoji cha Janga ,kata ya Janga ambazo zipo eneo hatarishi nyakati
za mvua .
Aidha imetoa
tahadhali na kuweka wazi kuwa hawatotoa kibali kwa wakazi hao ambao
nyumba zao zipo kwenye hatari ya kusababisha madhara wakati wa mvua
zinazoendelea kunyesha ama zijazo.
Akitoa
rai hiyo ,wakati alipokwenda kwenye kusimamia zoezi la kuweka X kwenye
nyumba hizo ,mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,alisema
zilizowekwa X ni 50 na nyingine zimeshindwa kufikiwa kutokana kuwa
katikati ya maji ya mvua.
Alieleza
, wananchi walioguswa wawe na amani na kuondoa hofu juu ya zoezi
zililowapitia na badala yake wasubiri kusikia jibu la maamuzi ya
serikali .
Hata hivyo ,Assumpter alisema kwasasa watatoa maeneo bure kuwahamisha wakazi hao ambapo watatakiwa kujenga wenyewe.
"Serikali
haijawahi kuumiza wananchi wake ,kuweni na subira ,tunaangalia cha
kufanya kwasasa na kusubiri majibu ya wataalamu wetu kuona itakavyokuwa"
"Wale
ambao nyumba zao zipo kwenye maji kabisa msijidanganye mtapewa kibali
kabisa ,kuhusu kuweka mtaro wa kutoa maji msikurupuke subirini
wataalamu"
"Wataalamu
tutawachukua wizarani na hao ndio watatujibu kama inawezekana kuweka
mtaro huo ,msije kutia fedha halo,Msijichangishe kwasasa hadi wataalamu
waseme majibu yao" alifafanua.
Assumpter
alieleza endapo wataalamu watasema kunahitajika zaidi ya mil.200 ni
vyema fedha hizo zitumike kwenye ujenzi mahala watakapohamishiwa .
Pamoja na hayo ,aliwataka kuondoka kwasasa kupisha mvua kwani amekuta mtu yupo kama ufukweni jambo ambalo ni hatari .
Pia
mkuu huyo wa wilaya ya Kibaha ,alisema mtumishi yeyote atakaeenda
kuwachangia chochote wasikubali labda kama mtumishi huyo atakuwa na
barua itaonyesha imetoka ofisini kwao.
Nae
afisa ardhi halmashauri ya Kibaha ,Frenk Mwalembe ,alisema amepokea
agizo la kuweka X nyumba hizo kutoka kwa mkuu wa wilaya ili kujua idadi
ya nyumba ambazo zipo eneo hatarishi .
Alisema
miaka ya nyuma eneo hilo lilikuwa linachimbwa visima ,ni eneo ambalo
maji hayana njia ya kutokea kwa wakati mmoja" na eneo hilo lipo nje ya
utaratibu wa mipango miji, "alisema Mwalembe.
Mwalembe alisisitiza kwamba, ni vyema wakazi hao wakaondoka ili kuondokana na kero wanayoipata .
Mkazi
ambae amekumbwa na adha hiyo ,luteni kanali mstaafu wa jeshi Angolile
Mwakajinga ,aliomba serikali ikubali wachangishane kuweka mtaro mkubwa
wa kudumu utakaopeleka maji mto Mkalamo .
Alisema
gharama ni kubwa lakini ni vyema kuweka mtaro huo kuliko hasara ya
kupewa viwanja bure ambapo watahitajika kwenda kujenga nyumba upya
wakati wengine uwezo huo hawana.
Nyumba
zaidi ya 30 zimezungukwa hadi sasa bila kuwa na njia ya kutoka maji
ambayo yametokana na mvua zilizonyesha wiki hii, kitongoji cha Janga.



0 Comments