Random Posts

RC Tabora: Viongozi Msigeuze Ushirika Kuwa Kichaka cha Kuficha Maovu

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri  akifungua Mkutano wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo Aprili 12,2018 wilayani Igunga.
 Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo (wa pili kushoto) akichangia mada kwenye  Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo.Wengine ni Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri(kushoto) Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo  Lazaro Ngullo(wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Nzenga Godfrey Ngupula(kulia)
 Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule (kushoto)akitoa ufafanuzi  kwa viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa wakulima wa Pamba kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo. Wengine ni Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri(katikati) na Mkuu wa Wilaya John Mwaipopo(kulia)
 Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo  Lazaro Ngullo(kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kufungua  Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama hicho uliofanyika mjini Igunga jana.Wengine ni Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri(kushoto) na Mkuu wa Wilaya John Mwaipopo(katikati)
Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Pamba ambavyo ni wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo  wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 22 uliofanyika mjini Igunga.

NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
 
SERIKALI imewaonya Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika Mkoani Tabora ambao wanafikiri wanaweza kugeuza Ushirika kuwa maficho ya kuwanyonya wakulima kuondoka mara moja kabla ya hatua kali hazichukuliwa dhidi yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo.

Alisema kiongozi aliye madarakani ajipime kama ni safi na mwadilifu  na sio kuwa kama kibaka mzoefu.
Mwanri aliongeza kuwa watu wanaofanya ujanja ujanja kwa ajili ya kutaka kuwanyonya wakulima wawachukulie hatua mapema kabla ya mambo hajaharibika.

Alisisitiza kuwa kila kiongozi ajifikie moyoni mwake kama kweli anaweza kuwa msafi ndio awe kiongozi.
Aidha Mkuu huyo Mkoa alisema maelekezo ya serikali ni kwamba pamba yote itauzwa kupitia ushirika na sio vinginevyo kwa kuwa lengo ni kutaka mkulima asinyonywe.

Alisema ushirika ndio njia pekee inayokuwa njia pekee ya kuwashika mkono wakulima wanyonge.
Naye Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule alisema kuwa kiongozi yoyote aliyewania uongozi kwa ajili ya maslahi binafsi ni vema ajiondoe mapema katika Ushirika ili asije akajikuta sehemu mbaya.

Alisema kiongozi atakayekutwa akiwa amegeuza Ushirika kama sehemu ya kupatia fedha kinyume cha Sheria atakamatwa na hataachiwa na atashitakiwa kama mhuhujumu uchumi.


Aidha Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule aliwataka viongozi wa Ushirika kutoishia katika kukaa Ofisini bali nao walime pamba ili wakulima wengine waende kujifunza jinsi ya kulima vizuri.

Post a Comment

0 Comments