Random Posts

Sekretarieti ya Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Yakutana na Naibu Spika wa Bunge la Uganda.Sekretarieti ya Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Yakutana na Naibu Spika wa Bunge la Uganda.

 Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Demetrius Mgalami (wa pili kushoto) kabla ya ujumbe ulioongozwa na Katibu huyo kuzungumza nae ofisini kwake Bungeni Mjini Kampala. Kushoto ni Wakili Dunford Mpelumbe, Afisa wa Chama hicho Tawi la Afrika
 Wajumbe wa Sekretarieti Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, waliongozwa na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha hicho Ndg. Demetrius Mgalami (kulia) mara baada ya ujumbe wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama Kanda ya Afrika ulipomtembelea Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah (hayupo kwenye pichani) na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Bungeni Mjini Kampala
 Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Demetrius Mgalami (kulia) akizungumza pale alipomtelea Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah (hayupo kwenye pichani)   ofisini kwake Bungeni Mjini Kampala. Kushoto ni Wakili Dunford Mpelumbe, Afisa wa Chama hicho Tawi la Afrika.
Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah (wa pili kulia), Mbunge wa Bunge la Uganda na Mweka Hazina wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Elijah Okupa (kulia), Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika  Ndg. Demetrius Mgalami (wa pili kushoto) na Wakili Dunford Mpelumbe (kushoto) afisa wa Chama hicho Tawi la Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ujumbe wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama Kanda ya Afrika kumtembelea Mhe. Naibu Spika na kufanya nae maongezi Ofisini kwake Bungeni Mjini Kampala.

 (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Post a Comment

0 Comments