Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema serikali itawafikisha
Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki wananchi wote wanaomiliki ardhi ambao
wamekuwa hawalipi kodi ya ardhi.
Lukuvi ametoa kauli
hiyo mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa watendaji wake ambapo
amesema serikali inapoteza mapato mengi kwa kuwa baadhi ya wananchi kukosa
uaminifu wa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo,
Waziri Lukuvi amesema ameamua kutoa muda hadi Aprili 30, 2018 ili kila mtu
anayemiliki ardhi awe amekwisha lipa kodi hiyo na kwa wale ambao hawatalipa
kodi kwa wakati ni wazi serikali itawafikisha mahakamani, kuwafutia hati za
viwanja hivyo na kuviuza upya kwa wamiliki wengine ama kuuza nyumba zao.
Aidha Mhe. Lukuvi
amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika
zoezi hilo ili kupunguza ukubwa wa kazi na kukusanya fedha kwa wakati na
kuongeza pato la taifa.

0 Comments