Rasheed
Taher aiingiza Tanzania kwenye nchi zilizowahi kuwa washindi
Kampala, Paris, 13 April 2018 – Tanzania imevunja rikodi kwenye Tuzo za kimataifa za wanafuzi
zijulikanazo kama DStv Eutelsat Star Awards baada ya mwanafunzi Taher
Rasheed kutoka shule ya Al-Madrasat Us-saifiyatul Burhaniyah ya Dar es salaam
kushinda nafasi ya kwanza katika category ya poster (bango) baada ya mchuano
mkali na mamia ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika.
Kwa upande wa insha mshindi alikuwa Amos
Mumbere kutoka shule ya Ntare nchini Uganda
Tuzo hizi ambazo zinahusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango
vyenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa
wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19 kote
barani Afrika ambapo kampuni ya MultiChoice inaendesha shughuli zake.
Mwaka huu, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango kuhusu
manufaa yaliyoletwa na uvumbuzi wa setelaiti katika maisha ya kila siku hapa
ulimwenguni na ni jinsi gani setelait imekuwa kama kiungo muhimu kwa shughuli
zote zinazofanyika kote duniani.
Taher alitangazwa rasmi jana jioni jijini Kampala nchini Uganda ambapo
jopo la watahini maarufu lilikaa na kupitia kazi za wanafunzi kutoka nchi
mbalimbali za Afrika. Jopo hilo liliongozwa na Paolo Nespoli, mwanaanga nguli
kutoka European Space Agency (ESA).
Akiongea baada ya kupokea habari hizo za ushindi, Taher amesema amefurahi
sana kwa ushindi huo mkubwa ambao umemletea yeye, shule yake na taifa zima kwa
ujumla sifa kubwa. “Nimefurahi sana kupokea taarifa hizi nzuri.
Naamini ushindi wangu utakuwa ni chachu kubwa
kwa wanafunzi wenzangu kote nchini kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika
tuzo kama hizi na mashindano mengine ya kitaaluma ya ndani na nje ya nchi”
alisema Taher.
Ameongeza kuwa kwa ushindi huu ni dhahiri kuwa wanafunzi wa Tanzania wana
uwezo mkubwa wa kushiriki na kushindana katika yanja ya taaluma ya sayansi na
pia inadhihirisha kuwa vijana wetu wana uwezo mkubwa hivyo tunatakiwa
kuhakikisha kuwa vipaji hivi vinakuzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya taifa
letu” alisema Maharage.
Mshindi wa bango atajishindia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini na
kutembelea kituo cha anga cha nchi hiyo na pia makao makuu ya MultiChoice
Africa akiwa kama mgeni maalum.
Shule zitakazotoa washindi
hao zitapata zawadi ya kufungia huduma ya DStv bure.
........................
About Eutelsat
Founded in 1977, Eutelsat Communications is one of the world’s leading
satellite operators. With a global fleet of satellites and associated ground
infrastructure, Eutelsat enables clients across Video, Data, Government, Fixed
and Mobile Broadband markets to communicate effectively to their customers,
irrespective of their location.
Over 6,700 television channels operated by
leading media groups are broadcast by Eutelsat to one billion viewers equipped
for DTH reception or connected to terrestrial networks. Headquartered in Paris,
with offices and teleports around the globe, Eutelsat assembles 1,000 men and
women from 32 countries who are dedicated to delivering the highest quality of
service.
For more about Eutelsat go to www.eutelsat.com
About MultiChoice Africa
Entertainment is a powerful way to tell stories that open our minds,
bring people together around shared passions, and connect us to new realities.
It makes us laugh and cry.
It informs, it educates and it inspires.
MultiChoice is a video entertainment company, and our purpose is to enrich
lives.
We make the best in entertainment
accessible to millions of households in 49 countries across Sub-Saharan Africa.
We do this through cutting-edge technology on our DStv and GOtv platforms –
delivering the content our customers love and contributing to the success of
local economies.
Born and bred in Africa, we are rooted in the countries where
our customers live.
We are managed and run by local
people, and strive to provide all our employees with new opportunities.
We’re proud of the contribution we make to our
communities, and our business has grown hand-in-hand with local economies by
forging long-term partnerships with governments, national broadcasters and
entrepreneurs. We want to use our


0 Comments