Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), na Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi,
wakionesha mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34
kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu
wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), na Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi,
wakibadilishana mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi
bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi,
yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), na Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakisaini
mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili
ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa
51 kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, akisalimiana na mwenyeji
wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al
Suwaidi, alipowasili Makao Makuu ya Mfuko huo Mjini Abu Dhabi, kwa ajili
ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya
shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi
Malagarasi yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, akiteta jambo na
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al
Suwaidi, kabla ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye
thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza
hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (wa tatu kushoto), akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif
Al Suwaidi, kabla ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye
thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya
Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
kulia kwake ni Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu,
Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk na Mkuu wa Dawati la Abu Dhabi kutoka Wizara
ya Fedha na Mipango, Bw. John Kuchaka.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), akisindikizwa
na Mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi,
Mhe. Saif Al Suwaidi, baada ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti
nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza
hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
………………
Benny Mwaipaja, Abu Dhabi
Tanzania imeendelea kuaminiwa na
Jumuiya ya Kimataifa ambapo Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Falme za
Kiarabu-Abu Dhabi, umeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola
za Marekani milioni 15, sawa na shilingi bilioni 34 za Tanzania, kwa
ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi yenye urefu wa
kilometa 51, kwa kiwango cha lami
Hafla fupi ya uwekaji saini wa
mkataba huo imefanyika katika makao makuu ya Mfuko huo yaliyopo Abu
Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo Mhandisi Mussa Ibrahim
Iyombe, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa-TAMISEMI, amesaini kwa niaba ya Serikali, na Mhe. Mohamed Saif Al
Suwaidi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi kwa niaba ya
Mfuko huo.
Akizungumza baada ya kusaini
Mkataba huo, Katibu Mkuu-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe, amesema kuwa
barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa ni kiungo kikuu cha usafiri wa abiria
na mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Kigoma na nchi jirani
za Burundi na Kongo DRC.
Amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa
kuboresha barabara hiyo kwa kiwango cha lami umelenga kuchochea uchumi
wa nchi kwa kuwezesha usafirishaji wa mazao ya wakulima pamoja na
kupunguza gharama na kuongeza uwezo wa kufanya biashara na nchi hizo
jirani.
“Tutabakiwa na kipande cha
barabara yenye urefu wa kilometa 28 kutoka Urambo hadi Kaliua na
kilometa 42 kutoka Chagu hadi Kazilambwa, barabara ambazo Serikali
inaendelea kuzitafutia fedha ili kukamilisha barabara yote inayoelekea
ukanda huo wa kati kutokea Dar es Salaam, Manyoni (Singida), Tabora hadi
Kigoma” Alisema Mhandisi Iyombe.
Ameushukuru Mfuko huo kwa
kuendelea kuiamini Serikali na kutoa mkopo huo wenye masharti nafuu
baada ya kufanya hivyo hivi karibuni kwa kutoa mkopo mwingine wa dola
milioni 57, uliofanikisha kuboreshwa kwa barabara ya Kidahwe hadi Uvinza
yenye urefu wa kilometa 77 kwa kiwango cha lami.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi, kwa upande wake,
amesema kuwa Mfuko huo uko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania
katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Amefafanua kuwa mradi huo ambao
mkataba umesainiwa mjini Abu Dhabi, utakuwa ni wa nne kufadhiliwa na
Mfuko wake Tangu uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Tanzania
uanzishwe mwaka 1977, ukiwemo mradi wa kuendeleza kiwanda cha Sukari
cha Kagera, Mradi wa Maji Vijijini huko Viwani Zanzibar na Mradi wa
kuboresha barabara ya Kidahwe hadi Uvinza kwa kiwango cha lami.
Kwa upande wake, Balozi wa
Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Mbarouk Nassor
Mbarouk amesema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni kiashiria cha
kukubalika kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Magufuli, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ya haraka
na kuungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.
“Hatua hii ni uthibitisho wa
mahuasiano mazuri ya kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Umoja wa
Falme za Kiarabu uliodumu kwa muda mrefu tangu mwaka 1977” Alisisitiza
Mhe.Mbarouk
Mhe. Mbarouk amebainisha kuwa
kukamilika kwa barabara hiyo ya Uvinza hadi Malagarasi kutachochea
maendeleo ya kiuchumi na mapinduzi ya viwanda kwa kuunganisha shughuli
za kiuchumi kama vile kilimo na maliasili pamoja na kukuza utalii.







0 Comments