Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipokea kompyuta 25 zenye
thamani ya shilingi milioni 45 kutoka kwa Mkuu wa Operesheni wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) zilizotolewa na Mfuko huo kwa ajili ya shule za
sekondari za jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akisikiliza kwa
makini maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mkugwa Mwalimu Salome
(kushoto) kuhusu mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya masomo ya sayansi kwenye moja
ya maabara ya shule hiyo jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akikagua majengo ya mabweni
ya Sekondari ya Wasichana ya Mkugwa wakati wa ziara yake shuleni hapo jimboni
kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma
Nembo ya Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) iliyowekwa kwenye kompyuta 25 zenye thamani ya
shilingi milioni 45 zilizotolewa kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Atashasta Nditiye kwa ajili ya shule za Sekondari zilizopo jimboni
kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisalimiana na wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Boni Consilii alipowasili kuzungumza nao wakati wa ziara
yake jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amepokea kompyuta 25 zenye
thamani ya shilingi milioni 45 kutoka kwa Mkuu wa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)
Mhandisi Albert Richard kwa ajili ya shule za Sekondari zilizopo Wilayani
Kibondo mkoani Kigoma ili ziwawezeshe wanafunzi na waalimu kujifunza na
kufundishia na kwenda sambamba na ulimwengu wa kisasa wa sayansi na teknolojia.
Mhandisi Richard
amesema kuwa ugawaji wa kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 45 kwa shule
za sekondari za Wilaya ya Kibondo ni mpango wa UCSAF kupitia Mradi wa
Kuunganisha Mashule.
“Tunaamini kuwa
kompyuta hizi zitasaidia kuinua elimu katika mkoa wa Kigoma na katika jimbo
zima”, amesema Mhandisi Richard.
Nditiye ameishukuru
UCSAF kwa kutoa kompyuta 25 kwa ajili ya shule za sekondari za jimboni kwake
Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma.
Ameshukuru kwa kupata msaada huo kwa ajili ya
shule mbalimbali ambazo zipo katika Wilaya ya Kibondo ambapo zitasaidia kuiweka
wilaya hiyo na shule hizo katika masuala ya mawasiliano kwa urahisi zaidi.
“Hizi
kompyuta zitawasaidia na kuwafanya wanafunzi wajifunze kwa kukiona kitu moja
kwa moja na waweze kufanya mawasiliano kwa urahisi zaidi,” amesema Nditiye. Amewashukuru
UCSAF kwa huduma nzuri wanazozifanya kwa shule na kwa taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine
Nditiye ametembelea shule ya sekondari ya Wasichana ya Mkugwa na ya Kibondo
ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha sita ya shule hizo.
Pia, alikagua miundombinu ya mabweni, madarasa, vyoo, maabara, viwanja vya
michezo na mahali pa kulia chakula kwenye shule hizo na shule ya Boni Consilii
zilizopo kwenye jimbo lake la Muhambwe wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Nditiye amewashukuru
wanafunzi na waalimu kwa kusoma kwa bidii na kufundisha kwa uzalendo ambapo imeiwezesha
Wilaya ya Kibondo kushika nafasi ya kwanza katika ngazi ya mkoa wa Kigoma,
nafasi ya nane kitaifa kati ya kumi bora katika halmashauri zote 187 zilizopo
nchini.
Amewaasa wanafunzi
waliohitimu kidato cha sita kwenye sekondari hizo kuwa wamebakiza muda mfupi
kuwepo shuleni ambapo mara baada ya mitihani ya taifa, watarejea kwa wazazi na
walezi wao na watajiunga na jamii ambapo hamna waalimu wala walinzi wa kufuatilia
mienendo yao.
Pia, kwa wale watakaobahatika kufaulu na kuendelea na masomo ya
chuo kikuu wawe makini na mienendo na tabia zao na wazingatie masomo kwa kuwa
ufaulu wao unategemea kujisomea kwa bidii.
Ameongeza kuwa wazazi
na walezi wawe karibu na wahitimu hao mara warejeapo nyumbani na watenge muda
kuzungumza nao mara kwa mara ili waendelee kuwasihi na kuwaonya wajiepushe na
vishawishi ili waweze kufikia ndoto zao kwa manufaa yao, familia zao na taifa
kwa ujumla ili Serikali ipate wataalamu wa kutosha kuendesha viwanda vyetu
kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa nchi ya viwanda na
yenye wataalamu wa kutosha kuendesha viwanda hivyo.
Imetolewa
na kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 Comments