Sura ya kivuko cha
miti kinachotumika kuvuka wakazi wa kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na
Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo ambapo kwasasa ujenzi wa daraja umeanza
utakaogharimu mil.100.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo, umeanza utakaogharimu mil.100.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo, umeanza utakaogharimu mil.100.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi kuhusu ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo.( Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
UJENZI
wa daraja litakalounganisha kata ya Pangani ,Wilaya ya Kibaha na Mpiji
Magohe wilaya ya Ubungo umeanza ambapo hadi kukamilika kwake utatumia
zaidi ya sh. milioni 100.
Akizungumza
na wananchi kwenye eneo la ujenzi Diwani wa kata ya Pangani Agustino
Mdachi alisema, tayari ujenzi umeanza na wameshaweka mawe ambayo
yatatumika kama kitako cha daraja kwa kutumia waya ili kuzuia
mmomonyoko.
Alieleza,
mawe yanayotakiwa ni malori 100 na nyaya hizo kwa ajili ya kuweka
kitako cha daraja upande wa Pangani na Mpiji Magohe .
"Baada ya hapo vitalazwa vyuma kwa ajili ya daraja"
“Tumeanza
ujenzi ambapo ujenzi wa daraja utafanywa na jeshi ambao tuliwaomba
daraja na sasa wameshakubali ambapo mawe yameshawekwa wao wakija
wataanza kuweka vyuma vya daraja,” alisema Mdachi.
Alisema
,gharama za ujenzi zinafanywa na wananchi ,kila kaya inatakiwa kutoa
kiasi cha sh. 10,000 na kuwataka wananchi kujitolea ili kukamilisha
ujenzi huo.
“Tumekubaliana
kwenye vikao vya wananchi kuwa kila kaya itoe kiasi hicho lakini kama
mtu anauwezo anaweza kutoa zaidi na tunawaomba wadau mbalimbali
wajitokeze kutusaidia kukamilisha ujenzi huu ambao utasaidia kuondoa
adha kwa wakazi wa kata ya Pangani,” alisema Mdachi.
Aidha
alisema kuwa, kwa kaya ambayo itashindwa kutoa mchanago huo makubaliano
watakapofikishwa kwenye ofisi za mtaa itabidi watoe kiasi cha shilingi
50,000 kama adhabu.
“Tunawaomba
wale wenye maeneo yao huku na wanakaa jijini Dar es Salaam wanapaswa
nao kuchangia ujenzi huo na endapo watashindwa kufanya hivyo watapaswa
kulipia na faini kwani wamekuwa hawaonyeshi ushirikiano kwa kuwa hawakai
maeneo hayo,” alisema Mdachi.
Alibainisha
wananchi wa kata hiyo wanategemea huduma za kijamii Mpiji Magohe ambako
ni jirani kuliko kufuata huduma Kibaha kwenye umbali wa zaidi ya
kilometa nane.



0 Comments