Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist
Ndikilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya uhamasishaji wa
kununua na kutumia dawa zinazozalishwa katika kiwanda cha Tanzania Biotech
Product Ltd kilichopo Kibaha, itakayofanyika april 12 mwaka huu ,huko Mailmoja.
Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, Yudas Ndungile
(wa kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika kikao
kilichokiitisha mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo (wa
kushoto)kuelezea kampeni ya uhamasishaji wa kununua na kutumia dawa
zinazozalishwa katika kiwanda cha Tanzania Biotech Product Ltd kilichopo
Kibaha, itakayofanyika april 12 mwaka huu ,huko Mailmoja
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Pwani wakimsikiliza kwa makini mkuu
wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo ,ofisini kwake wakati alipokuwa
akielezea kampeni ya uhamasishaji wa kununua na kutumia dawa
zinazozalishwa katika kiwanda cha Tanzania Biotech Product Ltd kilichopo
Kibaha, itakayofanyika april 12 mwaka huu ,huko Mailmoja
Picha na Mwamvua Mwinyi
……………………
Na Mwamvua
Mwinyi,Pwani
VIFO vinavyotokana na ugonjwa wa malaria katika mkoani Pwani, vimepungua
kutoka 124 kwa mwaka 2016 na kufikia vifo 57 sawa na asilimia 9.6 mwaka
2017.
Pamoja na hilo ,kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2015 -2017
wagonjwa wa malaria walioripotiwa katika zahanati ,vituo vya afya na hospitali
mkoani humo ,walikuwa 720,181.
Hayo yalibainika katika kikao cha mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist
Ndikilo ,kilichomkutanisha na waandishi wa habari ,kuelezea kampeni ya
uhamasishaji wa kununua na kutumia dawa zinazozalishwa katika kiwanda cha
Tanzania Biotech Product Ltd kilichopo Kibaha, itakayofanyika april 12 mwaka
huu ,huko Mailmoja .
Alieleza ,kutokana na takwimu hizo ugonjwa huo bado ni
hatari hivyo wamejipanga kuhamasisha na kuongeza matumizi ya dawa ya
viuadudu ili kudhibiti mbu waenezao malaria.
“Kwa kuzingatia kwamba kiwanda cha dawa hizi kipo hapa kwetu na kuwa
maambukizi ya malaria kimkoa bado yapo juu takriban asilimia 15 zaidi ya
maambukizi ya kitaifa ambayo ni asilimia 14, tumedhamiria kuongeza
matumizi ya dawa hiyo”
“Kwa uzoefu kwa wenzetu nchini Cuba ambao walianza kutumia viuadudu vya
kuua mbu wa malaria kabla yetu wamefanikiwa kutokomeza kabisa gonjwa hilo ”
alisema Ndikilo.
Ndikilo alisema ,katika uhamasishaji huo wanakusudia kufanya mambo mawili
ikiwemo kuujuliaha umma kuwa dawa ya kutokomeza malaria ipo Kibaha kwa kutoa
elimu kwa vitendo ya matumizi na kuzigawa dawa hizo bure kwa baadhi ya
wananchi.
Alifafanua dawa hizo zitakazogawiwa bure zimenunuliwa na Jumuiya ya
wafanyabiashara Mkoani Pwani kwa gharama ya milioni 1.056 ili wananchi hao
waondokane na malaria .
“Lengo la kampeni hii ni muendelezo wa utekelezaji wa agizo la Rais
dkt.John Magufuli alilolitoa wakati wa ziara yake kiwanda hicho June 22 mwaka
jana ,ambapo aliagiza kila halmashauri Tanzania Bara kununua dawa hii na
kuipulizia kwenye maeneo yenye mazalia ya mbu “alifafanua.
Hata hivyo ,Ndikilo aliagiza wakurugenzi wa halmashauri zote na wananchi
kujitokeza kukunua dawa ili kupambana na mbu kwenye maeneo yao.
Nae mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, Yudas Ndungile ,alisema licha ya
takwimu kuonyesha ugonjwa wa malaria kushuka kimkoa lakini jamii iendelee
kujikinga na kutumia njia nyingine kama dawa ,vyandarua ili kukabiliana
na ugonjwa huo.
Alielezea ugonjwa unaoongoza kwa sasa kimkoa ni magonjwa yanayotokana na
mfumo wa hewa ,ikifuatiwa na malaria.
Ndungile alisema ,mwaka 2016 ugonjwa wa malaria ulikuwa ukiongoza lakini
kwasasa umeshuka na kuwa wa pili hivyo kuonyesha idadi ya vifo navyo kupungua.



0 Comments