Random Posts

Wafanyabiashara Waungana Kumuaga Bi Lin Xiuling Jijini Dar es Salaam

Ndugu jamaa na marafiki waliungana pamoja na jamii ya wafanyabiashara kutoka nchini China kutoa salamu zao za mwisho wakati wakimuaga Bi Lin Xiuling (45) mke wa mfanyabiashara raia wa China anayefanya shughuli zake kariakoo jijini Dar es salaam.
 Bi Lin Xiuling aliuwawa nyumbani kwake Karikaoo na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi mnamo Marchi 13, 2018 majira ya asubuhi.
Majonzi vilio na huzuni zilitawala kwa waombolezaji pale katika viwanja vya Mnazi mmoja  Dar es salaam ambapo watu waliungana pamoja katika ibada ya kutoa heshima zao za mwisho na kumuaga Bi Lin.
Marehemu alikuwa ni mfanyabiashara kutoka katika jimbo la Fu Jian nchini China, alikuja Tanzania mnamo tarehe 8 March ili kuungana na mumewe katika kufanya biashara. Bi Lin ameacha mume na  familia ya watoto wawili.
Akizungumza mwenyekiti wa jumuiya ya wachina wanaofanya biashara kariakoo Bwana Xu Huo Pao, alisema Lin alitoka China kuja Tanzania kufanya biashara ya kuuza mapazia na vyandarua ambapo ndoto yake ilikatishwa ndani ya siku 24 tu tangu alipowasili nchini hapa.

Katika Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Lin Xiuling Mkuu wa wilaya ya Ilala  Sofia Mjema ameliomba jeshi la polisi kuharakisha uchunguzi wa mauaji hayo na kuhakikisha waliohusika wanapatikana.
 “Jitihada zimefanyika na hadi sasa amepatikana mtu mmoja kati ya wawili wanaosadikika kufanya mauaji hayo” alisema  Mjema.
 Pia amewaomba wafanyabiashara kutoka China na nchi mbalimbali kuwa waangalifu katika biashara zao na kujiwekea ulinzi wa kutosha  katika utunzaji wa mali zao hasa fedha nyingi wawe na utaratibu wa kuhifadhi benki pia amewashauri kuomba jeshi la polisi kuwapa ulinzi katika kusafirisha mali hizo.
 Sofia Mjema aliwaambia wafanyabiashara hao kutoka China kuwa serikali itahakikisha kuwa wanafanya biashara zao kwa utulivu na Amani.

Post a Comment

0 Comments