Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya Mji wa
Kibaha ,Leah Lwanji (wa kushoto )akipokea zawadi kutoka kwa kikundi cha
Pwani Generation Queens ,wakati wa sherehe yao ya mwaka mmoja ya
kikundi,wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa kikundi hicho Betty
Msimbe.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation Queens, Betty Msimbe (wa kulia)akizungumza wakati wa sherehe ya kikundi hicho kufikisha mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation Queens, Betty Msimbe (wa kulia)akizungumza wakati wa sherehe ya kikundi hicho kufikisha mwaka mmoja.
Baadhi ya wanachama wa kikundi
cha Pwani Generation Queens wakifungua shampen wakati wa sherehe ya
kusheherekea mwaka mmoja wa kikundi hicho. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
AFISA
maendeleo ya jamii katika halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji
amewataka wanawake kuacha kulalamika kukosa fursa ya mikopo ngazi ya
halmashauri na badala yake wajiunge kwenye vikundi ili kuwezeshwa
kirahisi.
Aidha
ametoa rai kwa wale wanawake wajasiriamali waliopiga hatua kiuchumi na
wenye uwezo kuthubutu kuwekeza kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na
hata vikubwa .
Leah
alitoa rai hiyo wakati wa sherehe za kufikisha mwaka mmoja wa kikundi
cha Pwani Generation Queens- Kibaha mkoani Pwani, ambacho kina
wanachama 75 hadi sasa.
Alieleza
wakati umefika kwa wanawake wajasiriamali kukimbilia fursa,kujikubali
,kujiamini na kuthubutu ili kujiinua kimaendeleo na kuacha utegemezi
ndani ya familia.
Leah
alisema ,wapo baadhi ya akinamama wajasiriamali wadogo ambao bado
hawajanufaika na fungu la asilimia 10 ya mapato ya ndani ambalo
hukopeshwa wanawake,vijana,wazee na walemavu.
"Hakuna mtu ama mjasiriamali mmoja mmoja atakaepewa fedha hiyo mkononi bila utaratibu wowote "
"Nawaomba
tusilalamike na kutupia lawama halmashauri,serikali,taasisi binafsi
pekee ,kwani utaratibu wa kupata fedha hizi unajulikana ,ni lazima
muungane vikundi ,muache ubinafsi ili hali mpate fursa hii kirahisi"
alisisitiza Leah.
Afisa
maendeleo huyo ,alielezea idara hiyo kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo wameweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajasiriamali 751
ambapo kati yao wanawake ni 480 .#
Hata hivyo Leah alisema, mwaka 2016-2017 halmashauri ilitoa fedha kiasi cha sh.mil .173
kwa ajili ya mikopo kwa wanawake na vijana ,2017-2018 ilitoa mil.368
na July -Sept 2017 walitoa mil.100 kwa vikundi 50 vyenye wanachama 320.
Aliupongeza muungano huo ,na kuwaomba wazidi kuwa wamoja ,waache majungu na fitna kwa lengo la kusonga mbele,kuinua umoja wao.
Mwenyekiti
wa Pwani Generation Queens ,Betty Msimbe alisema wapo kikatiba ,wana
akaunti na fedha ya akiba sh. mil .Tisa huku wakiendelea na miradi
midogo .
Alisema wanachama wake ni kuanzia miaka 18 na kuendelea wakiwa ni wakazi wa maeneo ya wilaya ya Kibaha,Kisarawe na Ubungo .
Betty alisema, lengo la kikundi ni kushirikiana katika mipango ya kimaendeleo, shida na raha na kuwezeshana.
Mwanachama wa kikundi hicho ,Zarina Zenzele alisema endapo watashirikiana wanaamini nia na malengo ya kikundi yatafikiwa.
Aliomba serikali na taasisi mbalimbali za kijamii kuwaunga mkono ili waweze kuwezeshwa na kupiga hatua kiuchumi.



0 Comments