Na Mwandishi Wetu
Wanchi wa
kata ya Ilala tawi la msimbazi mivinjeni wameiomba serikali kuwasaidia kutatua
kero za miundombinu zinazowakabili
ikiwemo ujenzi wa barabara na mifereji ya kupitisha maji ili waweza
kuwafikisha wagonjwa hospitalini.
Hayo
yamejiri kwenye mwendelezo wa ziara ya chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Ilala
ya kutembea kata na mashina yake ambapo Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ubaya
Chuma amesemakuwa kero hizo watahakikisha zinatatuliwa na viongozi wa maeneo
hayo akiwemo mbunge na diwani wake.
Aidha
wananchi hao wameiomba serikali pia kuwasaidia kupata ufumbuzi wa upatikanaji
wa mikopo haswa kwa kinamama na vijana ili waweza kuendeleza biashara zao na
kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande
mwingine wakazi wa tawi la shauri moyo wamekiomba chama Cha mapinduzi
kuwasaidia kutatua kero wanayokumbana nayo ya kujaa mtope katika soko la ilala
na maadhi ya mifereji katika eneo hilo kujaa maji.
Akizungumza
katika tawi hilo Katibu Muenezi CCM wilaya ya Ilala Said Side amewataka wakazi
hao kuwa wavumilivu kwani Manispaa la Ilala imeandaa mchakato wa kuboresha
masoko yote yaliyopo ndani ya wilaya hiyo.
"
Tayari soko ya kisutu liko kwenye marekebisho na jitihada za seriali zipo za
kutosha kwani tumeongea na Diwani wa eneo hili na fedha za kurekebisha masoko
mengine tayari zishatengwa" amesema side.



0 Comments