NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI kupitia Shirika lake la la Ugavi wa
Umeme Tanzania(TANESCO) itajenga Kituo kidogo(sub station) mpakani wa Urambo na
Kaliua na kingine kitajengwa unapokaribia kuingia Nguruka kwa ajili ya
kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa Wilaya hizo na maeneo
jirani.
Kauli hiyo ilitolewa Aprili 16, 2018 na Waziri wa Dkt. Medard Kalemani wakati alipotembelea
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya
kuanza ziara yake ya siku moja mkoani
humo kukagua miradi ya usambazaji umeme vijijini.
Alisema kuwa lengo la ujenzi wa vituo hivyo
ni kurekebisha hali ya upatikanaji wa umememe na kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika
ambao utawawezesha wananchi kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji bila
wasiwasi.
Katika hatua nyinginye Waziri wa Nishati alisema Serikali itaendelea kuwatembelea
Wakandarasi waliopewa jukumu la kujenga miundo mbinu ya kusambaza umeme vijiji
chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu ili kuhakikisha
wanakamisha kazi kama walikubaliana katika mkataba.
Alisema wamewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza
Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kuhakikisha wanawasha walau vijiji vitatu kili wiki kwa ajili
kuharakisha upelekaji wa umeme kwa wananchi waliopo maeneo ya vijijini.
Aidha
alisema utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwepo na vijiji 1541
ambavyo vilikuwa havizaingizwa katika Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu na hivyo vitaingizwa mwakani ili
navyo viweze kuangashiwa umeme.
Waziri
huyo wa Nishati aliagiza wananchi wapatiwe umeme katika maeneo yote ya vijiji ambayo
tayari kuna miundombinu ya umeme inapita bila kusubiri Mradi
Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu.
Akisoma
taarifa ya Mkoa . Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Nathalis Linuma alisema
kuwa katika REA III jumla ya vijiji 162 vitanufaika na huduma ya umeme kwa
mzunguko wa kwanza.

0 Comments