Subscribe Us

header ads

Hakuna mtoa huduma atakaetoa huduma za maabara bila kusajiliwa- Dkt Charles Massambu

 Mwenyekiti wa Baraza la wataalamu wa maabara  Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto, Viola Msangi akifungua kikao kifupi cha kutoa taarifa huduma na majukumu za maabara kwa watanzania (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa, Dkt Charles Massambu, kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam Mei 22, 2018.
 Msajili wa Baraza la wataalamu wa maabara, Theophil Malibiche akielezea muundo wa Baraza hilo  na majukumu yake wakati wa kikao cha kutoa taarifa kuhusiana utoaji huduma za maabara kwa watanzania kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam Mei 22, 2018.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Charles Massambu akizungumza na waandishi wa habari   katika ofisi  ndogo za wizara hiyo Jijini Dar es Salaam Mei 22, 2018 wakati wa kikao cha   Baraza la wataalamu wa Maabara kuhusiana na huduma za zinazotolewa na Baraza hilo. 
 Msajili wa Baraza la wataalamu wa maabara, Theophil Malibiche akielezea muundo wa Baraza hilo  na majukumu yake wakati wa kikao cha kutoa taarifa kuhusiana utoaji huduma za maabara kwa watanzania. 
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la wataalamu wa maabara, Dr. Edda akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
 Mkuu wa Huduma za Maabara Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto, Dickson Majige (kushoto) pamoja na wajumbe wataamu wa maabara wakiwa katika  kikao kifupi cha kutoa taarifa huduma na majukumu za maabara kwa watanzania
Seemu ya waandishi wa habari wakiwa katika kikao hicho.
Picha na Philemon Solomon
Mkurugenzi Msaidizi Huduma ya uchunguzi na magonjwa kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Charles Massambu ( kushoto) akisisitiza juu ya umuhimu wakujisajili katika huduma za maabara (kulia) Mwenyekiti wa Baraza la wataalamu wa maabara, Viola Msangi.
..........................
Na Happy Daudi-Mtazamo News

Baraza la Wataalam wa Maabara nchini limewataka watoa huduma za kimaabara kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa na vibali kwani kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa wa sheria.

Mkurugenzi Msaidizi Huduma ya uchunguzi na magonjwa kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Charles Massambu amesema sheria itachukua mkondo wake kwa wale wanaotoa huduma kwa wananchi  za kimaabara bila  vibali vya kusajiliwa.

 Ameyasema hayo wakati wa kikao cha waandishi wa habari kutoa taarifa kuhusu majukumu na kazi zinazotolewa na baraza hilo kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam Mei 22, 2018.

"Hakuna mtoa huduma atakaetoa huduma za maabara bila kusajiliwa tukibaini tutachukua hatua za kisheria," amesema Dk. Massambu.

Massambu amesema baraza linatambua uwezo na utaalamu katika kuelimisha jamii ya watanzania kuhusu majukumu katika kuwahudumia na changamoto za majibu ya vipimo kutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine Wizara imechukua hatua ya uhakiki wa ubora wa vipimo.

"Tanzania kuna maabara 33 ambazo ni nyota moja mpaka nne,nyingine nane zilizo na hadhi ya kimataifa ambapo vipimo vyake huwa ni sawa na vya nchi nyingine za nje.

Akifafanua Vigezo vya maabara amesema  katika ngazi ya taifa na kanda vibali vimetolewa na Shirika la Afya Duniani ambapo waliamua kutoa nyota za viwango vya ubora hatua kwa hatua.


Ameviomba vyombo vya habari kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na madhara ya matumizi ya maabara ambazo hazisajiliwa na baraza hilo ili kuwasaidia wananchi kupata vipimo sahihi pamoja na kuwapunguzia gharama za matibabu.

Kwa upande wa Msajili wa Baraza hilo Theophil Malibiche amesema kisheria zipo gharama kidogo zinazoendana na usajili wa wataalamu wa maabara ambazo zimegawanyika katika usajili wa awali na wa kudumu kwa kiwango tofauti cha elimu ada ya kila ambayo kila mwaka.

Post a Comment

0 Comments