Random Posts

Halmashauri Mkoani Tabora Zatakiwa Kutenga Vituo Vingi vya Upimaji VVU na Ushauri Nasaha

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri  akizungumza na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI wakati akifunga mkutano wa siku moja siku moja uliofanyika mjini hapo ulio chini ya Mradi wa SAUTI unalenga kuhakikisha hakutakuwepo na maambukizi mapya ifikapo mwaka 2030.
 Mkuu wa Wilaya Quuen Mlozi akitoa maoni yake jana mjini Tabora wakati wakati wa mkutano wa siku moja wa wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI  chini ya Mradi wa SAUTI unalenga kuhakikisha hakutakuwepo na maambukizi mapya ifikapo mwaka 2030.
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega  Godfrey Ngupula (kulia mstari wa mbele)  , Mkuu wa Wilaya ya Abel Busala (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri (kushoto) na viongozi wengine walionyuma yao wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) wakati wa kufungua mkutano wa siku moja wa wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI 
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa(kulia mstari wa mbele)  na Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo(kushoto mstari wa mbele) na viongozi wengine walionyuma yao wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) wakati wa kufungua mkutano wa siku moja wa wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI 
 Baadhi ya washiri wa mkutano wa siku moja  wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) wakati wa kufungua mkutano huo  wa wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
 Baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri mbalimbali mkoani Tabora wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) wakati wa kufungua mkutano huo  wa wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI ulifanyika jana. Walio nyuma yao ni wajumbe wa mkutano huo.
Meneja Mwandamizi Utekelezaji wa Mradi wa SAUTI kutoka Shirika la Jhpiego Nelson Rutabanzibwa akizungumza jana mjini Tabora na waandishi wa habari juu ya malengo ya  mradi huo ambao unalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 watu wote waliopata ushauri nasaha na kupima na kugundulika wana maambukizi wawe wanajua hali zao na wale wanatumia dawa za kufubaza VVU.

NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
6 May 2018
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halamashauri zote kuhakikisha wanatenga maeneo mengi kwa ajili ya uanzishaji wa vituo ambavyo wananchi watakwenda kupata ushauri nasaha na kupima kwa hiari ikiwa ni sehemu ya kujinga na UKIMWI.

Alitoa wito huo jana mjini Tabora wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwenye mkutano wa siku moja.

Alisema hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya kutoa elimu katika maeneo mengine yenye mkusanyiko wa watu wengi juu ya kujikinga kwa wale ambao bado hawajapata maambukizi na wale ambayo tayari wapate dawa za kufubaza virusi(ARVs).

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema utafiti ubaini kuna mwako mdogo kwa wanaume kupima na kutumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARVs) na kutoa wito kwa wanaume kujenga tabia kuongozana na wake zao katika kwenda kupata ushauri nasaha na kupima VVU.

Alisisitiza woga wa baadhi ya wanaume unaweza kikwazo katika mapambano dhidi ya Ukimwi katika jamii.

“Baadhi ya wanaume wengi wanaogopa kwenda kupima…mara nyingi wanasubiri majibu ya wake zao wakiona amepata majibu kuwa hana maambukizo naye anaamini kwamba yuko salama , jambo ambalo linaweza lisiwe kweli…ni vema elimu itolewe ili wenza waende kupima wote” alisema Mwanri.

Naye Meneja Mwandamizi Utekelezaji wa Mradi wa SAUTI kutoka Shirika la Jhpiego Nelson Rutabanzibwa alisema mradi huo unalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 watu wote waliopata ushauri nasaha na kupima na kugundulika wana maambukizi asilimia 90 wawe wanajua hali zao na wale wanatumia dawa za kufubaza VVU , hatua itakayosaidia kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Rutabanzibwa aliongeza kuwa mradi huu unalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 kusiwepo na vifo vinavyotokana na Virusi vya Ukimwi, unyanyapa usiwepo na hakuna maambukizi mapya.

Alisema mradi huu unalenga kusaidi juhudi za Serikali katika mwitikio dhidi ya VVU hasa kwa makundi maalumu yaliyo kwenye hatari ya kupata maambukizi ama kuambukizwa kama wale wanafanya biashara ya mapenzi.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Tabora Queen Mlozi aliwawataka wadu mbalimbali kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili wajitokeze kwa wingi katika maeneo yao kupima na kujua afya zao.
Mradi wa SAUTI unaratibiwa na  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa(TAMISEMI)  na kutekelezwa na Shirika la jhpiego kwa kushirikiana na  mashirika ya Engender  Heath, Pact Tanzania na NIMR tawi la  Mwanza chini ya ufadhili wa Mfuko wa dharula wa Rais wa Marekani wa kupamana na UKIMWI kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID) .

Mradi huo ambao ni miaka mitano unatekelezwa katika mikoa 14 na Halmashauri 51 ya Tanzania Bara.

Post a Comment

0 Comments