Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami pamoja na viongozi wengine wa jumuia hiyo wa hapa nchini wakati kiongozi huyo alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisalimiana na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Viongozi wa Jumuia ya Kihindu (BAPS) wakijadili jambo wakati Kaimu kiongozi wa Dunia wa Jumuia hiyo Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji.

Kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami akimpa zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati kiongozi huyo alipotembelea nchini hivi karibuni. Tangu mwaka 2016
BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo
hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea
vizuri.
Picha na JKCI
Na
Mwandishi Maalum,
Jumuia ya Kihindu Tanzania (BAPS) imetoa
kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo ziatumika kwaajili ya kulipia
gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto wenye matatizo hayo hapa nchini.
Fedha hizo ambazo zitatumika kwaajili ya upasuaji wa moyo kwa
watoto 30 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimetolewa
hivi karibuni na kaimu kiongozi wa Dunia wa jumuia hiyo.
Akizungumza kuhusu msaada huo Kaimu kiongozi wa Jumuia
ya Kihindu Duniani Mtukutu Bhaktipriyadas
Swami alisema wametoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia jamii yenye uhitaji hasa watoto wanaosumbuliwa
na maradhi ya moyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi alishukuru kwa msaada huo na kusema
kuwa fedha zilizotolewa zitatumika kwa walengwa ambao ni watoto wanaotakiwa
kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Prof. Janabi alisema kuwa Taasisi hiyo imekuwa na
uhusiano mzuri na Jumuia ya BAPS ambao
kila mwaka wamekuwa wakichangia fedha kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto
ambao baada ya matibabu wamepona na wengine wamerudi shuleni kuendelea na masomo yao.
Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa
ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290
wameshafanyiwa upasuaji.

0 Comments