Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima
la Taifa la Tanzania(NIC) Sam Kamanga akimkabidhi mifuko ya saruji kwa
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe,Hamis Dikupatile baada ya mbunge
wa viti maalum mkoani Pwani ,Zainab Vullu kupokea msaada huo kutoka kwa
Mkurugenzi huyo
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima
la Taifa la Tanzania,(NIC) Sam Kamanga ,akizungumza jambo wilayani
Kisarawe Mkoani Pwani .
Mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani
,Zainab Vullu akiongea na baadhi ya madiwani na watendaji halmashauri ya
Kisarawe (hawapo pichani)
Na Mwamvua Mwinyi- Kisarawe
SHIRIKA
la Bima la Taifa la Tanzania (NIC) ,limetoa msaada wa mifuko ya saruji
160 ,yenye thamani ya zaidi ya sh.mil.mbili ,wilayani Kisarawe Mkoani
Pwani .
Msaada huo umelenga
kusaidia kumalizia miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya umma
ikiwemo zahanati ,vituo vya afya na mashule katika kata zilizopo
wilayani humo .
Akikabidhi
msaada huo kwa mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani Zainab Vullu
,mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa la Tanzania, Sam
Kamanga ,alisema shirika hilo linatoa misaada ya aina hiyo kwenye maeneo
mbalimbali nchini yenye changamoto za kijamii .
Alieleza msaada huo ni moja ya kati ya shughuli za shirika za kurudisha kwa jamii.
"Katika
mpango kazi wetu tumejiwekea kuwa na wananchi katika changamoto zao,Hii
ni miongozo ya utawala bora kwa kuwa karibu na jamii ,tunatekeleza,
tumeenza mkoani Iringa ,Mwanza ,Sumbawanga katika sekta ya afya na
elimu " alieleza Kamanga.
Akipokea
msaada huo ,mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab alishukuru
shirika hilo na kusema aliongea nao juu ya ombi hilo na anashukuru
amesaidia .
Alisema mifuko hiyo ya saruji inaelekezwa katika kata zinazoendelea na ujenzi wa miradi ya elimu na afya.
Zainab
alitaja kata hizo kuwa ni pamoja na Msimbu mifuko 20, Mafizi mifuko 30,
Vihingo mifuko 30 ,Chole mifuko 10,Marumbo 10,Kazimzumbwi 10, Kiluvya
10 ,Vikumburu 10 ,Msanga 10 na kata ya Masaki mifuko kumi .
"Ndondo
si chululu ,hiki tulichokipata kwangu ni kikubwa ,nawashukuru NIC kwani
itakwenda kuboresha ujenzi wa mashule ,vituo vya afya na zahanati"
alieleza Zainab .
Mbunge
huyo viti maalum Mkoani hapo ,alisema kuwa ,adhama ya serikali ni kuinua
uchumi wa Viwanda na Viwanda bila waajiriwa wenye afya njema sio jambo
jema .
Zainab alisema madarasa yakikamilika pia huku wanafunzi wakiwa na afya njema,kwa hakika inapendeza ,alisisitiza"
Aliwataka
madiwani kutumia saruji hiyo kwa matumizi lengwa badala ya kuiacha bila
kutumia kwa wakati na matokeo yake ije kuharibika .
Zainab
aliliomba shirika hilo kuendelea kuwasaidia hasa kwenye upande wa
vikundi vya wanawake na vijana ili viweze kujiinua kiuchumi .
Nae
mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe ,Hamis Dikupatile alisema kwasasa
wilaya ipo katika mkakati wa kuondoa 0 mashuleni hivyo aliwaomba wadau
na shirika hilo kuangalia namna ya kuwezesha sekta ya elimu ili
kuondokana na kushuka kitaaluma .
Dikupatile alimshukuru mbunge Vullu na NIC kwa jitihada zao na kuwaomba wasichoke kuitupia macho wilaya hiyo .
Alisema wilaya ya Kisarawe inaendelea kupigania maendeleo na kuinuka kiuchumi kwa maslahi ya jamii na kuondokana na umaskini .




0 Comments