NA TIGANYA
VINCENT
25 May
2018
MKUU wa
Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametanga kiama kwa watu wote wanaoshiriki kuwaoza
watoto wadogo wakiwemo wa Shule kwa kuwakata na kuwafikisha Mahakamani ili
waweze kuadhibiwa.
Hatua hiyo
inalenga kukomesha mimba na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike ikiwa ni sehemu
ya kutetea haki za watoto wa kike kupata elimu kama walivyo wavulana na vile
kuokoa maisha yao ambayo yanaweza kupotea wakati wa kijifungua kwa kuwa bado ni
wadogo.
Mwanri alitoa amri hiyo jana katika
vijiji vya Wilaya ya Igunga na Urambo mbalimbali wakati wa kampeni yake ya
kutokomeza ndoa na mimba za utotoni.
Aliwaagiza Vyenyeviti wa Serikali za Mitaa , vijiji au kuanza mara moja zoezi la kuwakamata watu
wote ambao wataokutwa wakila wali au
kushabikia sherehe za ndoa ambayo Bibi harusi ni motto mdogo au mwanafunzi.
Mwanri alisema ni jambo la aibu
kuona mfumo wa serikali upo kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa lakini bado
Tabora inaendelea kutajwa kuwa miongoni mwa vinara wa mimba na ndoa za utotoni.
Mwanri alisema kuwa kiongozi wa
ngazi yoyote akiwemo polisi akikuta kuna harusi ya mtoto aliye chini ya miaka
18 awe mwanafunzi au sio akamate watu wote wanaosherekea tukio hilo haramu kwa
sababu linarudisha nyuma juhudi za kumkomboa mtoto wa kike kutoka mfumo dume.
“Ukifika katika harusi kabla ujaanza
kula chakula ulinza binti aliyefunga ndoa ana umri gani…kama ni chini ya miaka
18 usile chakula ondoka…OCD , Mtendaji ukikutana aliyefungishwa ndoa ni chini
ya miaka 18 …wapambe somba… mashangazi somba…bibi harusi na bwana harusi somba”
alisisitiza
“Waliokula ubwabwa somba…aliyebeba
ubwabwa wa harusi hiyo na kupeleka kwake somba…tutachambua mmoja baada ya mmoja
ili kujua mwenye hatia na asiye na hatia tutamwachia ili watu wanyoke na waache
kuwafuata watoto wadogo”alisema .
Mkuu huyo wa Mkoa alisema ili
kuepuka kuingia katika matatizo ni vema vijana na watu wazima wanaonyemelea
watoto wa kike na wale wanaoshabikia ndoa za utotoni kuacha mara moja na kutoa
taarifa kwa mamlaka husika wanapoona mtu mwenye tabia chafu kama hizo ili awe
kuchukuliwa hatua.
Alisema akiwa amepewa dhamana ya
kuongoza Mkoa wa Tabora hatakubali kuendelea kupata aibu ya kunyoshewa vidole
kwa mambo mabaya kama vile kuongoza katika mauaji , watoto kuwa watoro , mimba
na ndoa za utotoni.
Mwanri aliwaonya viongozi na
watendaji ambao watashindwa kusimamia utekelezaji wa kukomesha tabia hizo
atawachukulia hatua ikiwemo kuwasimamisha na hatimaye kupendekeza wafukuzwe
kazi ambao wako katika Mamlaka za juu.

0 Comments