Baadhi ya viongozi wa shule ya sekondari Zogowale ,serikali ya mtaa wa
Zogowale na halmashauri ya Mji wa Kibaha wakiwa pamoja na mkurugenzi wa
taasisi ya Rehema Foundation ,Mohammed Cesur ,wakifurahia uzinduzi wa
mradi wa maji shuleni hapo ,baada ya kujengewa kisima cha kupampu
kilichogharimu zaidi ya sh.mil.11 .
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Zogowale ,mjini Kibaha Mkoani
Pwani ,wakishangilia kupata huduma ya maji shuleni hapo ,baada ya
kujengewa kisima cha kupampu kilichogharimu zaidi ya sh.mil.11 ,(wa
katikati)Mkurugenzi wa Rehema Foundation ,Mohammed Cesur .
(Picha na
Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
CHANGAMOTO
ya maji safi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa shule ya sekondari
Zogowale ,Mjini Kibaha mkoani Pwani ,inabaki historia baada ya kujengewa
kisima kirefu cha kupampu ,kilichogharimu zaidi ya sh.mil 11, kwa msaada kutoka taasisi ya Rehema foundation.
Licha ya hilo ,shule hiyo bado inakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa uzio hali inayotishia usalama kwa wanafunzi na walimu .
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya kisima hicho ,kaimu mkurugenzi wa Rehema
Foundation ,Rafii Jongo ,alisema ujenzi wa kisima hicho umekamika kwa
wiki mbili .
Alielezea
,taasisi hiyo inajihusisha na masuala ya kijamii na hadi sasa
imeshasaidia kuchimba visima ndani ya jamii 185 Tanzania Bara na
Visiwani ambapo kwa mkoa wa Pwani imechimba visima 50.#
"Tunatoa
pia misaada ya chakula na kugawa nyama ya ng'ombe kwa watu wasiojiweza
nyakati za mfungo tatu ,Na kila mwaka tunachinja ng'ombe 1,000,
tunapeleka watanzania kusoma masomo mbalimbali nchini Uturuki" alisema
Jongo .
Nae
Mkurugenzi wa taasisi hiyo ,Mohammed Cesur aliwataka wanafunzi watunze
kisima hicho kwa ajili ya manufaa ya shule na jamii inayowazunguka.
Aliwaasa wanafunzi wajitahidi kusoma ili kuinua taaluma zao .
Cesur alisema, changamoto ya maji itakuwa imekwisha hivyo anaamini wanafunzi hao wataelekeza juhudi zao katika masomo .
Kwa
upande wake ,mkuu wa shule ya sekondari ya Zogowale ,Tatu Mwambala
alisema awali walikuwa wakitumia visima vilivyopo nje ya shule na katika
mradi wa kijiji .
Alisema maji yalikuwa si ya uhakika na sio salama ambako walipoteza muda kutafuta maji .
Tatu alielezea ,ipo changamoto nyingine kubwa ya ukosefu wa uzio hali inayosababisha kushindwa kuwa na usalama wa kutosha.
"Tumeanza
kujenga uzio kwa jitihada za wazazi na jamii ,tumekwama kifedha
,tunaomba wadau watusaidie kwa ari na mali kumalizia ujenzi huo "
"Shule hii ina wanafunzi wa kike ambapo inatakiwa wawe kwenye usalama zaidi kuliko shule kuwa haina uzio"alisisitiza Tatu .
Mwanafunzi
wa kidato cha tano shuleni hapo ,Shamim Shomvi alisema, walikuwa
wakipata shida ya maji na kusababisha kutumia muda mwingi kwenda
kutafuta huduma hiyo badala ya kujisomea.
Alisema,
walitumia maji ya visima vya chini ambayo hayakuwa salama, " wanafunzi
wengine waliugua magonjwa ya matumbo kama typhoid".
Shamim aliwashukuru Rehema Foundation, na kuwaomba wasisite kuwasaidia kutatua matatizo mengine yanayowakabili .
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jennifer Omolo aliwasihi kuutunza mradi huo ili udumu katika kipindi kirefu.



0 Comments