Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihutubia washiriki wa hafla ya
uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi .
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula akihutubia washiriki wa wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma ambapo Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) alikuwa mgeni rasmi .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akisisitiza kuhusu fursa zilizopo Mkoani Dodoma wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dustan Kitandula akizungumzia manufaa ya kuanzishwa kwa Tume ya Madini wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki Kuzindua Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula wakati akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi vitendea kazi Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Shukrani Manya mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga ( kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Aderladus Kilangi( kulia) Wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya madini leo Jijini Dodoma.
Makamishana wa Tume hiyo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi Vitendea kazi mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Dkt. Florence Turuka ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki wakati wa hafla ya kuzindua Tume hiyo iliyofanyika leo Jijini Dodoma.

Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Anjelina Mabula akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO , Dodoma)
Frank Mvungi-
MAELEZO, Dodoma
Tume ya Madini
imetakiwa kuhakikisha inatekeleza
kikamilifu jukumu la usimamizi, Udhibiti, Ukaguzi, Ufuatiliaji, Ukusanyaji wa
taarifa na kuweka kumbukumbu kwa kusimamia sekta hiyo kwa uadilifu hali itakayosaidia Taifa kunufaika na uwepo wa
rasilimali madini.
Akizungumza wakati
akizindua Tume hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki
amesema kuwa kuzinduliwa kwa Tume hiyo
kunaashiria kuanza kwa ukurasa mpya katika sekta ya madini nchini kwa
kuwa uamuzi huo ni mapinduzi makubwa
hali itakayosaidia wananchi kunufaika na sekta hiyo.
"Ni imani yangu,
na pia ni imani ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na imani ya
Watanzania wote kuwa mtatubadilishia simulizi za sekta ya madini kutoka kuwa za
kukatisha tamaa na kuwa za matumaini, kuibadili historia ya sekta ya madini
kutoka kuwa ya miguno na manunguniko na kuwa yakujivunia" Alisisitiza Mhe.
Kairuki
Akifafanua Mhe.
Kairuki amesema kuwa, si kwamba Tume hiyo imepewa mamlaka makubwa bali pia
imepewa imani kubwa kwa kuwa mamlaka makubwa yanakuja na wajibu mkubwa mikononi
mwa watendaji wa Tume hiyo.
Aliongeza kuwa
Watanzania wana matarajio makubwa na Tume hiyo na viongozi wake kwa kuwa
Serikali na wananchi wanaamini kuwa sekta hiyo sasa iko katika mikono safi na salama.
Kutokana na imani
hiyo Mhe. Kairuki amesema kuwa wananchi
wanaamini Tume hiyo itatenda haki, kusimamia ukweli na kuzingatia maslahi ya
kizazi hiki na kijacho ili viweze kunufaika na madini ambayo Mwenyezi Mungu amelijalia Taifa
letu.
Aidha, Mhe. Kairuki ameitaka Tume hiyo
kuhakikisha inasimia kikamilifu wachimbaji wadogo kwa kuwatambua na kurasimisha shughuli
zao ili sekta hiyo iwanufaishe kama
ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kwa upande wa vibali
vya mauzo ya madini nje ya Nchi amesema kuwa ni vyema Tume ikafanya mapitio ya fomu na vibali ili kuhakikisha kuna maelezo na
taarifa za kina za madini yanayosafirishwa kuhusu yalipotoka (origin),.
Vile vile kwa
kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ameitaka Tume iandae mbinu na mikakati ya
kudhibiti utoroshaji wa madini ili kudhibiti biashara haramu ya madini.
Tume ya madini
imetakiwa kuangalia uwezekano wa kuweka utaratibu wa kutoa bei elekezi za
madini ya aina mbalimbali ambapo utaratibu huo utawasaidia wachimbaji wadogo na
wa kati.
Pia Mhe. Kairuki
ameitaka Tume hiyo kuhakikisha
kuwa kila anayefanya biashara ya madini ana leseni na ni leseni hai iliyolipiwa
na kuhakikisha kwamba inathibiti watu au
makampuni yanayomiliki leseni walizopewa kwa muda mrefu bila kuziendeleza
kinyume na masharti ya leseni hizo.
Kuwepo kwa utaratibu
wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuona maendeleo ya uwekezaji katika migodi ambayo imepata leseni
ni moja ya jukumu ambalo Tume hiyo inatakiwa kulitekeleza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.
Idrissa Kikula amesema kuwa wamepokea
maelekezo yote ya Serikali na Tume hiyo iko tayari kufanya kazi kwa maslahi ya
Taifa .
Aliongeza kuwa Tume
imejipanga kuhakikisha kuwa inatatua migogoro iliyopo katika sekta hiyo kwa
kushirikisha vyama vyao vilivyopo katika maeneo yao.
Tume ya Madini
imeundwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa rasilimali za Taifa zinawanufaisha
wananchi wote, Kutokana na azma hiyo Tume imepewa jukumu la kusimamia sekta ya
madini na Wizara ya Madini kubaki na Masuala ya kisera.

0 Comments