Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 12:15 asubuhi katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo linalofanya safari zake kutoka Kigoma kuelekea Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi hilo.
Dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa waliofariki dunia, huku idadi ya vifo ikisemekana inaweza kuongezeka kutokana na hali mbaya za majeruhi.
Kamanda Otieno amesema jeshi lake linaendelea kushughulikia ajali hiyo na kwamba taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.
WATU saba wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma, asubuhi ya Juni 6, 2018.






No comments:
Post a Comment