Subscribe Us

header ads

KATIBU MKUU CCM PAMOJA NA WAJUMBE WA SEKRETARIETI WAANZA ZIARA MKOANI KAGERA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wajumbe wa Kamati ya Siasa ya mkoa wa Kagera kwenye ukumbi wa Kayago mara baada ya mapokezi alipowasili mkoani humo ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa yenye lengo la kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, leo Nyakanazi wilayani Biharamulo. (Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu (Bara) Ndugu Christina Mndeme wakati wa kikao cha kupokea taarifa za Chama na Serikali kwenye ukumbi wa Kayago mara baada ya mapokezi alipowasili mkoani Kagera ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa yenye lengo la kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, leo Nyakanazi wilayani Biharamulo, Kagera. (Picha na CCM Makao Makuu)
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya mkoa wa Kagera wakiwa kwenye ukumbi wa Kayago tayari Kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao wapo kwenye ziara yenye lengo la kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, leo Nyakanazi wilayani Biharamulo. (Picha na CCM Makao Makuu)

Post a Comment

0 Comments