Bi. Emmy Hudson Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) akitoa maelezo kuhusu Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya Miaka Mitano kwenye semina ya viongozi iliyofanyika leo mkoani Rukwa,Sumbawanga.
Mwakilishi wa UNICEF nchini anayeshugulikia Masuala ya Ulinzi wa Watoto Bi. Gillian San Aye akizungumza kwenye semina ya viongozi wa mkoa wa Rukwa kuhusu mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambapo amesema UNICEF itashirikiana na Tanzania kufanikisha zoezi hilo.
Bw. Rashid Maftah kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dodoma akizungumza kuhusu umuhimu wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa kutoa ushirikiano kwa RITA ili kuwezesha usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ufanikiwe na kuwa endelevu .Ametoa wito huo leo mjini Sumbawanga kwenye semina ya viongozi wa mkoa na wilaya iliyoratibiwa na RITA.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw. Denis Bandisa akizungumza mjini Sumbawanga kuhusu utayari wa halmashauri za Rukwa kushirikiana na RITA kufanikisha zoezi la usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano zoezi litalofanyika kwa wiki mbili kuanzia leo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joseph Mkirikiti (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Dini na wale wa Mila wa Mkoa leo mara baada ya semina ya viongozi kuhusu Mpango wa Usajili wa Watoto Walio na Umri Chini ya Miaka Mitano utakaofanyika na RITA katika halmashauri zote za Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joseph Mkirikiti (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa wa Sekretariati ya Mkoa leo mara baada ya semina ya viongozi kuhusu Mpango wa Usajili wa Watoto Walio na Umri Chini ya Miaka Mitano utakaofanyika kote mkoani Rukwa hivi karibuni chini ya RITA.
(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

0 Comments