Msajili
wa Bodi ya Wabuifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Arch. Edwin Nnunduma
akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa tatu wa mwaka wa Bodi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Dkt.
Ludigija Bulamile akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa tatu wa AQRB
jijini Dar es Salaam.
SERIKALI imewataka watà alamu wazawa wa ujenzi nchini kuungana ili kupata fursa za kushiriki miradi mbalimbali ya mkakati inayotekelezwa katika majenzi.
Pia ameitaka Bodi ya AQRB kupunguza gharama za usajili ili kuwezesha watu wengi zaidi kujisajili.
Akifungua Mkutano Mkuu wa tatu wa mwaka Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete alisema kuunganisha nguvu ya pamoja kwa wataalamu kutawezesha mitaji yao kuimarika na kuweza kupata kazi za ujenzi kwenye miradi mikubwa.
"Kumekuwa na malalamiko kadhaa kuwa serikalu imekuwa haiwashiriikishi wataalamu wazawa katika miradi mbalimbali ya kimkakati jambo ambalo siyo kweli kwani serikali imekuwa ikiwapa kipaumbele zaidi wataalumu wazawa hususani kipindi hiku cha serikali ya awamu ya sita'" alisema Mwakibete.
Alitolea mfano mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa serikali imewashirikisha wataalamu wazawa kwa kiasi kikubwa.
Aliongeza kuwataka wakadiriaji majenzi kuacha kufanya makadirio makubwa pale wanapopata fursa kwani wakifanya hivyo kumekuwa kukichangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kupata nafasi za kushiriki miradi mikubwa.
Akuzungumzia gharama za usajili aliwaasa kuangalia namna ya kufanya ilu kuwezesha wataalamu wengi zaidi kujisajili .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya AQRB Mbunifu Majengo Ludigija Boniface alisema lengo la mkutano huu ni kutathimini utendaji kazi pamoja na kuwanoa wataalamu ili waweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya ujenzi.
Alitaja mada kuu ya mkutano huo kuwa ni uhifadhi wa majengo katika maeneo ya mijini na barani Afrika.
Naye Msajili wa AQRB Arch.Edwin Nnunduma alisema bodi imesajili jumla ya wataalamu 1,329 Kati ya hao wataalamu wazawa ni 1,296 na wageni 34.
Allisema mwaka 2021/22 bodi ilipanga kukagua miradi 2,600 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara na kwamba hadi sasa tayari bodi imekagua miradi 3,172 ukaguzi huu unahakikisha wataalamu wa majenzi wanatumika kubuni kikamilifu na kusimamia majenzi ili kulinda ubora wa majengo na usalama wa Raia na Mali.




0 Comments