Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na
Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh nchini Misri tarehe 07 Novemba, 2022.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha
na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa
COP27 unaofanyika katika Mji huo nchini Misri tarehe 07 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye mazungumzo na Rais wa Malawi Mhe. Lazarus Chakwera katika ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh International Congress Centre
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi Wakuu wa nchi mbalimbali kabla ya kuanza kwa Mkutano wa
kujadili mabadiliko ya Tabianchi COP27 unaofanyika katika Mji wa Sharm El
Sheikh nchini Misri tarehe 07 Novemba,
2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakizungumza na viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa 27 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi COP27 unaoendelea katika Mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri tarehe 07 Novemba, 2022.






0 Comments