Tuesday 24 October 2023

Wadau wa Mitandao ya Kijamii wapewa elimu ya Kodi

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano la wadau wa mitandao ya Kijamii ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023, ambapo wadau hao watapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Wizara hiyo, na kujengewa uwezo hususan kwenye masuala ya Sheria mpya ya PPP, Muundo wa Wizara, Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini na Mafao na Pensheni.
Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mitandao ya Kijamii ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, Bw. Mathias Canal, akizungumza wakati wa kongamano hilo ambalo limekutanisha wadau wa mitandao ya kijamii mbalimbali, ambapo wamepata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Wizara hiyo, na kujengewa uwezo hususan kwenye masuala ya Sheria mpya ya PPP, Muundo wa Wizara, Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini na Mafao na Pensheni. Kongamano hilo la siku mbili linafanyika mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wadau wa Mitandao ya Kijamii, wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Afisa Utawala wa Wizara ya Fedha, Bw. Brighton Ngowo (hayupo pichani), kuhusu muundo wa wizara hiyo, wakati wa Kongamano la wadau hao ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, linalofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023, mkoani Morogoro.
Afisa Utawala wa Wizara ya Fedha, Bw. Brighton Ngowo, akizungumza kuhusu muundo wa Wizara ya Fedha wakati wa Kongamano la wadau wa mitandao ya Kijamii ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, linalofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023, mkoani Morogoro, ambapo wadau hao watapata fursa ya kujifunza masuala mengine mbalimbali kuhusu Wizara hiyo, hususan kwenye masuala ya Sheria mpya ya PPP, Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini na masuala ya Mafao na Pensheni.
Wadau wa Mitandao ya Kijamii, wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Afisa Utawala wa Wizara ya Fedha, Bw. Brighton Ngowo (katikati), kuhusu muundo wa wizara hiyo, wakati wa Kongamano la wadau hao ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, linalofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023, mkoani Morogoro.
Afisa Mitandao ya Kijamii kutoka Wasafi Media, Bw. Issa Lazaro, akichangia jambo wakati wa Kongamano la wadau wa mitandao ya Kijamii ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, linalofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023, mkoani Morogoro, ambapo wadau hao watapata fursa ya kujifunza masuala mengine mbalimbali kuhusu Wizara hiyo, hususan kwenye masuala ya Sheria mpya ya PPP, Muundo wa Wizara, Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini na masuala ya Mafao na Pensheni.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha, Morogoro)
....................................

Na. Joseph Mahumi, WF, Morogoro

Wadau wa Mitandao ya Kijamii wameaswa kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti halali zinazolingana na kiasi cha fedha walichotoa kila wanapofanya manunuzi na kutoa risiti wanapo uza bidhaa na huduma.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, wakati akifungua Kongamano la wadau wa mitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24 Oktoba, 2023.

Amesema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa njia ya kigitali ya kuifikia jamii kwa haraka na kwa ukubwa na amewaomba wadau hao kutumia fursa hiyo kuielimisha jamii umuhimu wa kulipa kodi ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo kwa wananchi.

“Wizara inawatambua nyie ni wadau muhimu sana naomba mkawe vinara wa kuelimisha jamii ili kuongeza elimu ya masuala ya kodi na kuelezea kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kusimamia uchumi na pia kuwaelimisha jamii kuhusu agenda ya maendeleo ya taifa na miradi inayotekelezwa na serikali kwa ajili ya maslahi ya watanzania ikiwemo miradi ya Kimkakati.” amesema Bw. Mwaipaja 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kongamano hilo, Bw. Mathias Canal ameipongeza wizara ya fedha kwa kuandaa kongamano hilo la siku mbili na kusema kuwa hiyo ni fursa ya kurahisisha utendaji kazi wao kwa umma haswa kwa kujengewa uwezo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Wizara ya Fedha.

Bw. Canal ameongeza kuwa, Wizara ya Fedha iendelee kuhakikisha inatoa ufafanuzi kwa umma kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na umuhimu wa mikopo ili kuondoa sintofahamu kwa jamii kuhusu mikopo ya serikali.

“Hongera sana Mkuu wa Kitengo cha Habari Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja kwa kubuni kongamano hili pia tufikishie salamu za pongezi kwa Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba kwa kukubali kufanyika kwa kongamano hili ambalo ni muhimu kwa wadau wanaohabarisha jamii” alisema Bw. Canal.

Kongamano hilo la Siku mbili linatoa fursa kwa wadau wa mitandao ya kijamii kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Wizara hiyo, na kujengewa uwezo hususan kwenye masuala ya Sheria mpya ya PPP, Muundo wa Wizara, Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini na masuala ya Mafao na Pensheni.

No comments:

Post a Comment