TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA)
Kampasi ya Singida imeendesha zoezi la uchangiaji kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko
yaliyotokea Katesh, wilayani Hanang mkoani Manyara.
Ambapo zoezi hilo limeenda sambamba
na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya
kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake.
Kampeni hii huwafanyika kuanzia
tarehe 25 Novemba na kumalizika kuanzia tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa
ajili yakupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON, DOTTO MWAIBALE-SINGIDA.
Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Bi. Flora
Lemunge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Desemba 9, 2023 katika
viwanja vya taasisi hiyo wakati wa zoezi la uchangiaji kwa ajili ya kusaidia waathirika
wa mafuriko yaliyotokea Katesh, wilayani Hanang mkoani Manyara.
Jeshi la polisi Singida pamoja na
wananchi,wasanii waliojitokeza katika zoezi hilo wakichangia damu kwaajili ya
waathirika wa mafuriko.
Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakiendele kuosha magari.
Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakitoa burudani wakati wa zoezi hilo.
Msanii wa Bongo Fleva H. Kelly Lamata
akiwa pamoja na msanii mwingine wakitoa burudani kama mchango wao.
Michezo ikiendelea kutoka kwa
wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida.
0 Comments