Subscribe Us

header ads

PPAA YAOKOA BILIONI 583 MICHAKATO YA ZABUNI ZA UMMA

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imefanikiwa kuzuia upotevu wa fedha za serikali takribani TZS: 583,591,615,609.00 katika mshauri 162 yaliyokuwa katika hatua mbalimbali za michakato ya ununuzi wa umma kwa kipindi cha miaka takribani miaka minne.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando alipozungumza na waandishi wa Habari pembezoni mwa Kongamano la 15 Wataalam wa Ununuzi Ugavi linaloendelea katika viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Jijini Arusha.

“Katika kipindi cha takribani miaka minne tumeweza kusikiliza mashauri 162 na baada ya kupitia mashauri hayo, tumezuia zabuni 35 zenye takribani ya billioni 583.5/- ambapo endapo zabuni hizo zingetolewa kwa wazabuni hao waliokosa sifa na hivyo kuisababishia Serikali hasara katika eneo hilo,” alisema Bw. Sando.

Aidha, Bw. Sando aliongeza kuwa PPAA imekamilisha mchakato wa kujenga moduli ya kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa njia ya kieletroniki katika mfumo wa Ununuzi wa Umma Kieletroniki (NeST), kinachosubiriwa ni kukamilika kwa Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma ambapo zipo katika hatua ya mwishoni.

Post a Comment

0 Comments