Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
........................................
Na Dotto
Mwaibale, Dar es Salaam
RAIS wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Sh. Bilioni 17
kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule mkoani Kilimanjaro.
Maboresho ya
shule hizo yanakwenda kufanikisha wanafunzi 30,901 kujiunga na kidato cha
kwanza Januari 2025 Mkoa wa Kilimanjaro.
Fedha hizo
zilizotolewa na Rais Samia zitatumika kuboresha miundo mbinu ya madarasa,
mabweni na ujenzi wa shule mpya 17 za sekondari.
0 Comments