Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) na Mkewe Salma Kikwete (kulia) wakielekea kupanda Treni ya Mwendo kasi ya SGR wakati wakielekea Jijini Dodoma kushiriki Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao utafanyika Januari 18 hadi 19, 2025. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.
...........................................
Na Dotto
Mwaibale, Dar es Salaam
WAJUMBE 600
wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Rais Mstaafu Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete wametia fora kwa kusafiri na treni ya Mwendo
kasi ya SGR kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Dodoma kushiriki mkutano huo
utakaoanza Januari 18 na 19, 2025.
Hali hiyo
imeonekana leo asubuhi Januari 16, 2025 katika Stesheni ya Treni ya Magufuli
Dar es Salaam ambapo kuanzia saa 12 hadi saa 2: 30 asubuhi wajumbe hao makundi kwa
makundi walifika katika stesheni hiyo na saa 3: 30 waliondoka kwa treni
maalumu kuelekea jijini Dodoma.
Mbali ya
wajumbe hao watu wengine walioondoka na treni hiyo kwenda kwenye mkutano huo ni
wasanii mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na
Mwanao, Steve Nyerere na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tukio hilo alisema jumla ya wajumbe 600 watasafiri kwa usafiri huo wa treni hiyo pamoja na wattu wengine jumla yao itakuwa ni 900.
“ Shirika letu limepewa heshima kubwa ya kuwasafirisha wajumbe hawa kwani wangeweza
kusafiri kwa ndege, mabasi na magari yao binafsi lakini kazi hiyo tumepewa
sisi,” alisema Kadogosa.
Alisema kwao
kusafirisha wajumbe hao sio mara ya kwanza kwani walishawahi kusafirisha
wajumbe kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na
kuwa kwa kuaminiwa huko na kutumi usafiri wao kwao ni fursa kibiashara.
Alisema
wajumbe ambao watatumia treni hiyo kusafiri kwenda Dodoma ni kutoka
Zanzibar, Mtwara, Lindi, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
“ Treni hii maalumu kwa ajili ya kusafirisha wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM haitaathiri ratiba za safari za treni za kila siku ambazo zitaendelea kama kawaida,” alisema Kadogosa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu safari hiyo ya wajumbe hao kuelekea Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao waliambatana na wajumbe hao kwenda Dodoma wakizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kabla ya kuanza kwa safari hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere akijadiliana jambo na wenzake Stesheni ya Treni ya Magufuli kabla ya kuanza safari ya kwenda Dodoma kushiriki mkutano huo.
Muonekano wa Treni Maalumu ya SGR ambayo inawabeba wajumbe hao wa mkutano mkuu wa CCM.
Baadhi ya wajumbe hao na abiria wengine wakisubiri kuondoka kuelekea Dodoma.
Wahudumu wa Treni ya SGR wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea Dodoma na wajumbe hao.
0 Comments