Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Januari 2, 2025.
...........................................
Na Mwandishi Wetu, Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa mwezi mmoja kwa Katibu
Tawala wa mkoa pamoja na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Katavi kufanya ukaguzi
wa kina kwenye maeneo ya biashara nakuchukua hatua za haraka Kuzuia magonjwa ya
mlipuko ambayo tayari yameathiri maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi.
Mrindoko ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake kabla ya kuelekea katika gereza la mahabusu Mpanda kwaajili ya kukabidhi
vitu mbalimbali ikiwemo mbuzi kwa lengo la kusherekea pamoja na mahabusu
sikukuu za mwaka mpya.
Mbali na tahadhari ya magonjwa ya mlipuko pia Mrindoko amebainisha mambo
mbalimbali ya kimaendeleo ambayo watayapa kipaumbele kwa mwaka huu 2025 ili
kuboresha huduma kwa wananchi pamoja na kuinua uchumi wao na mkoa kwa ujumla.
Mrindoko amesema moja ya mambo ambayo watayaangalia kwa jicho la kipekee ni
suala la umeme wa uhakika ili kuwapa fursa wananchi wandani na njee kuwekeza,
0 Comments