TANZANIA YANG’ARA UUNGANISHAJI MFUMO WA MUSE NA CS- MERIDIAN - MTAZAMO MEDIA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Thursday, 27 February 2025

demo-image

TANZANIA YANG’ARA UUNGANISHAJI MFUMO WA MUSE NA CS- MERIDIAN

Responsive Ads Here

4
1%20(1)
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya akifungua mafunzo kuhusu Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) iliyounganishwa, kwa Timu ya wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, yaliyofanyika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Dodoma.
-------------------------------------------

Na. Peter Haule na Asia Singano, Dodoma.
 
Tanzania imefanikiwa kuwa nchi ya kwanza kuunganisha Mfumo wa Usimamizi wa Madeni (CS- Meridian) na Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) kwa nchi za Afrika uliotambuliwa na Jumuiya ya Madola na kuifanya kuwa kitovu cha mafunzo ya Mifumo hiyo.
 
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, alipokuwa akifungua mafunzo kwa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya waliokuja nchini kujifunza namna Mifumo hiyo inavyofanya kazi.
 
Alisema kuwa Timu hiyo ya Wataalam imekuja ili kujadiliana na kujifunza katika maeneo ya Mifumo ya kuweka takwimu za masuala ya madeni kwa kuwa nchi hizo pia zinakopa kutoka kwa wadau mbalimbali, hivyo kutakiwa kuweka takwimu za ukopaji vizuri na kulipa madeni kwa wakati.
 
“Tunashukuru tumewapokea wajumbe hawa na sisi tutajifunza kutoka kwao namna wanavyofanya kazi, tunaona kwamba ushirikiano huu utakwenda vizuri na nisehemu tu ya mambo mengi ambayo tumekuwa tukiyafanya kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji na namna tunavyotoa huduma kwa watu wetu”, alisema Bw. Mwandumbya
 
Alisema kuwa Wizara ya Fedha itahakikisha mafunzo hayo yanaenda vizuri na malengo yaliyopangwa yanatimia ili nchi hizo ziweze kuboresha utendaji wake kwa upande wa kuweka takwimu sawasawa lakini pia kulipa madeni.
 
Mafunzo hayo yanasaidia kuwa waangalifu kwa upande wa kukopa na kuzisaidia nchi hizo kuwa salama kiuchumi na kuepusha madeni yanayoweza kuziletea changamoto za maendeleo ya kiuchumi.
 
Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Kenya, Jeremiah Tomno, alisema kuwa malengo makubwa ya ziara yao yalikuwa kujifunza namna Tanzania ilivyo unganisha Mfumo wa Muse, CS- Meridian na Benki Kuu.
 
Alisema kuwa kutokana na mawasilisho yaliyofanyika, wamejifunza mambo mengi hata waliyokuwa hawajayatarajia ambayo ni mambo mema kwao, na kwamba watawasilisha mada ambazo zitakuwa na manufaa kwa pande hizo mbili.
 
Bw. Tomno aliongeza kusema kuwa wanafanya hayo kwa kuwa nchi hizo zipo katika Jumuiya na Ukanda mmoja, hivyo wanahitaji kufanya mambo ambayo kwa kiasi kikubwa yanatakiwa yafanane kwa kuwa wawekezaji wanazitazama nchi hizo kwa namna inayofanana.
 
Alishukuru kwa niaba ya Timu yake kwa mapokezi na kwamba wamejipanga kuhakisha wanapata ujuzi wa kutosha na wanatoa pia ujuzi wao kwa manufaa ya pande hizo mbili.
 
Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. John Sausi, alisema kuwa baada ya Serikali kufanikiwa kuunganisha Mfumo wa MUSE na Mfumo wa Usimamizi wa Madeni, Jumuiya ya Madola, waliona utekelezaji na usimamizi wa deni kwa Tanzania umekuwa mzuri, jambo lililosababisha nchi nyingi kuja kujifunza Tanzania.
 
“Wizara ya Fedha imekuwa ikitekeleza maelekezo ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu kuunganisha Mifumo ambayo imekuwa ikitumika, ambapo Wizara ya Fedha imefanikiwa kuunganisha Mifumo mingi hadi sasa tangu maelekezo hayo yalipotolewa.
 
Alisema kuwa Wizara ya Fedha imeunganisha Mifumo kuanzia ukusanyaji wa mapato hadi namna mapato hayo yanavyotumika na hivyo kutokuwa na mwingiliano wa watu katika Mifumo hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *