Waziri wa Mambo ya Ndani Innocent Bashungwa (katikati) waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT) alipo mwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla ya futari kwa viongozi wa dini na wadau wa amani ilioandaliwa na JMAT jijini Dar es salaam.
.........................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JUMUIYA ya Maridhiano Tanzania (JMAT) imepongezwa kwa kuwa mstari wa mbele katika kutangaza amani na kutatua migogoro miongoni mwa watanzania bila kujali tofauti za kiimani, kisiasa au kijamii.
Waziri wa Mambo ya Ndani Innocent Bashungwa, amesema hayo wakati akimuwakilisha waziri mkuu kwenye hafla ya futari kwa viongozi wa dini na wadau wa amani ilioandaliwa na JMAT jijini Dar es salaam.
Bashungwa amesema tunajivunia mchango mkubwa ambao JMAT inautoa kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa na jamii iliyo na amani, utulivu bila kujali tofauti za kiimani.
Waziri Bashungwa pia amesema JMAT ni jumuiya inayoamini falsafa ya 4R ya Rais samia Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikisisitiza kujenga jamii yenye upendo, amani na mshikamano.
Vile vile Bashungwa amewataka waumini wa dini zote kuwa na matendo mwema katika kipindi hiki cha mfungo kuwa sehemu ya maisha yetu na kufanya Tanzania kuwa kisiwa cha amani.
Naye Mufti na sheikh mkuu
wa Tanzania Dkt Abubakar Zubeiry Bin
Ally, amewataka watanzania kulinda amani na kuepuka vitendo vinavyoweza
kuhatarisha uvunjifu wa amani na mshikamano uliopo nchini.
Waziri Bashungwa akikabidhiwa zawadi na viongozi wa JMAT.
No comments:
Post a Comment