WANANCHI NJOMBE WAIOMBA TANESCO, REA KUONGEZA KASI YA KUWAUNGANISHIA UMEME - MTAZAMO MEDIA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Wednesday, 19 March 2025

demo-image

WANANCHI NJOMBE WAIOMBA TANESCO, REA KUONGEZA KASI YA KUWAUNGANISHIA UMEME

Responsive Ads Here

PICHA%2001
Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Melela Mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi 2025.
PICHA%201
PICHA%202
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mathayo Davidi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtwango mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi, 2025.
PICHA%203
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatib Kazungu akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Lwangu Mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi 2025.
PICHA%204
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wakala wa Nishati Vijijini(REA), Mhandisi Jones Olotu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lupende Mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika vijiji vya Mkoa wa Njombe tarehe 18 Machi 2025.
PICHA%205

NJOMBE

Wananchi wa Mkoa wa Njombe ambao bado hawajafikiwa na huduma ya umeme wameiomba Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania  (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuongeza kasi ya  kuwaunganishia umeme katika kaya zao ili waweze kuutumia kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

 

Hayo yameelezwa kupitia Viongozi wa Vijiji  vya Melela, Mtwango, Lwangu, Lupende na Melela wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyolenga kukagua maendeleo ya  mradi wa usambazaji umeme vijijini katika vijiji vya Mkoa wa  Njombe tarehe 18 Machi 2025.

 

Viongozi hao wamesema wananchi wameingia hamasa zaidi ya kuunganishiwa umeme baada ya kuona maendeleo yanazidi kuimarika katika baadhi ya Kaya ambazo tayari zimeunganishiwa umeme.

 

Aidha, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ambayo  imetoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ukiwemo umeme katika maeneo yao ambapo kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakiona kasi kubwa ya maendeleo.

 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewatoa hofu wananchi hao kwa kuwaeleza kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha inafikisha umeme kwa wananchi wote ifikapo 2030.

 

Ameeleza  kuwa maendeleo katika maeneo yote hupelekwa kwa hatua kama ilivyo kwa miradi ya umeme lakini lengo la Serikali ni wananchi wote wafikiwe na huduma.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mathayo David amewasisitiza wananchi  kuendelea kutandaza nyaya katika nyumba zao ili miradi ya umeme uiakapowafikia waunganishwe kwa haraka.

 

Ameeleza kuwa,  wananchi ambao hawahitaji kusuka nyaya wafike katika ofisi za TANESCO Ili wapatiwe kifaa cha umeme tayari( UMETA) kwa gharama ya Shilingi elfu 27,000 tu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *