Na Christopher siwingwa
..............................................
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman JAFO,amewapongeza wanawake wajasiriamali wa Tanzania kwa kuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa katika sekta mbali mbali kwa kuinua pato la la Taifa.
Dkt Jafo amesema hayo wakati wa hafla ya tuzo za wanawake wajasiriamali kwenye sekta mbali mbali za Viwanda na Biashara, ilioandaliwa na chama cha wafanyabiashara wanawake na Viwanda (TWCC)
Waziri Jafo amewasifia wanawake na kusema Tanzania imepiga hatua kubwa katika uwakilishi wa mwanamke na idadi kubwa katika sekta mbali mbali za maendeleo.
Serikali imeweka mazingira yanayowezesha wanawake wajasiriamali kustawi kama viongozi na mawakala wa mabadiliko, uwezeshaji wa kiuchumi na msingi wa kishiriki kwao katika jamii." Amesema waziri Jafo.
Dkt Jafo amewahakikishia wanawake kuwa Tanzania imeendelea kuwapa nafasi za kuongoza na kuandika mwanzo mpya katika historia ya Tanzania na ni wakati wa kuvunja vikwazo na kuleta mabadiliko makunwa.
Naye mtendaji mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) Bi Anjelina Ngalula, amewataka wanawake wajasiriamali kuweka umuhimu wa kusajli biashara zao ili kwa mamlaka za serikali ili ziwe endelevu na kupata washirika kutoka medani za kimataifa.
Pia Anjelina amewaasa wanawake kuto kuwa na papara ya kusimamia biashara nyingi kwa wakati mmoja,kwani ni kikwazo na anguko la biashara zao.
Wajasiriamali wakiwa kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman JAFO akiwa kwenye hafla tuzo za wanawake wajasiriamali
No comments:
Post a Comment