Wizara ya Fedha imeungana na Watanzania wengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, iliyofanyika kitaifa Jijini Arusha, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza maadhimisho hayo yakiwa yamebeba kauli mbiu ya ‘’Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji’’.
Maafisa Hesabu Wakuu, Kitengo cha Huduma za Mfuko Mkuu (CFS), Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky na Bi. Mercelina Haule, wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amiri Abeid, jijini Arusha
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)
No comments:
Post a Comment