Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Dkt. Particia Laverley, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki hiyo inayofanyika Abidjan nchini Côte D’ivoire, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki na Tanzania, yatakayowasilishwa kwa Uongozi wa AfDB katika Mikutano ya Mwaka 2025.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Katibu Msaidizi wa Baraza la Mawaziri, Bw. Fidelis Mkatte pamoja na maafisa wengine waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania.

0 Comments