Na Christopher Siwingwa
Wakandarasi nchini wametakiwa kuwa waadilifu na weledi katika kutekeleza miradi na kukamilika kwa thamani ya fedha iliopangwa.
Wito huo umetolewa na mtendaji mkuu wa wa wakala wa bara bara nchini TANROADS , mhanfisi Mohamed Besta jijini Dar es salaam wakati akifunga mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2025.
Mhandisi Besta amewasisitiza na kuwakumbusha wahandisi na makandarasi kuwa wizara ya ujenzi inafanyia kazi changamoto zote zinazo wakabili ikiwemo ya kutolipwa kwa wakati katika miradi yao.
Bwana Besta amesema anaamini kuwa yapo mambo mengi ambayo wamejadiliana na utekelezaji Wake haujafika mwisho. Lakini serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan ni sikivu na inaendelea kuzifanyia kazi.
Naye makamu mwenye
kiti wa bodi ya usajili makandarasi nchini CRB, mhandisi Farida Mawenya,
ameitaka taasisi ya ya kudhibiti Manunuzi ya umma PPRA kuhakikisha utekelezaji
wa sheria na kanuni za upendeleo kwa maalum kwa wakandarasi wa ndani
unazingatiwa kikamilifu ilikushiriki kwa ukamilifu katika miradi ya ujenzi
nchini.


0 Comments