Subscribe Us

header ads

WAZIRI ULEGA AHIMIZA MUUNDO WA UTUMISHI KWA MAFUNDI SANIFU NCHINI

Na Christopher Siwingwa 

Wizara ya ujenzi ipo kwenye mchakato wa kuboresha muundo wa utumishi kwa MAFUNDI sanifu ili kuleta uwiano wa kimaslahi kati yao na wahandisi.

Waziri wa ujenzi Abdallah Ulega amesema hayo wakati akifunga mkutano wa saba wa wa mafundi sanifu uliofanyika jijini Dar es salaam, ambao ilioandaliwa na Bodi ya usajili wa wahandisi (ERB). kutoka sehemu mbali mbali nchini.

Mkutano huo umehudhuliwa na mafundi sanifu zaidi ya 800 pamoja na wadau wa sekta mbali mbali za Viwanda na kauli mbiu isemayo" Muundo wa utumishi kwa kada ya mafundi sanifu katika utumishi wa umma na sekta binafsi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, waziri Ulega amesema ameiagiza bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) kuongeza idadi kubwa ya ya usajili wa wahandisi wenye sifa sitahikihi za kitaaluma na ambao wana uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko la ajira katika miradi ya kimkakati hapa nchini.

Pia waziri Ulega amesema katika jitihada za kukuza uchumi, serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan itaendelea kuimarisha na kuboresha mazingira ya kibiashara ya wawekezaji katika Viwanda, hususani vile vinavyo tumia mali ghafi za ndani.

Kwa mfumo huo, bwana Ulega amewataka mafundi sanifu hao kuchapa kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa pamoja na kukamilisha miradi yao kwa wakati na kwa thamani iliyo halisi.

Naye msajili wa Bodi ya usajili wa wahandisi ERB, bwana Bernard Kavishe, amesema kuwa, mafunzo maalum yanayotolewa kwa mafundi sanifu ni endelevu yanayokusudia kuongeza weledi na ufanisi katika sekta hiyo muhimu.

Post a Comment

0 Comments