Bw. Julius Mbwiga, enzi za uhai wake
.......................................
Na Dotto Mwaibale
KATIBU wa Chama Cha Mapinzuzi (CCM) , Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe, Julius Mbwiga amefariki dunia leo Julai 6, 2025.
Kifo chake kimewasikitisha watu wengi waliokuwa wakimfahamu
kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.
Mbwiga amefariki dunia wakati akijiandaa kwenda kwenye kikao
cha kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani humo
ambacho kilipangwa kufanyika leo Julai 6, 2025.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa ndugu jamaa, marafiki na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Songwe.
No comments:
Post a Comment