Random Posts

KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHMAN KINANA AZUNGUMZA NA WANA KILOSA, AWASILI WILAYANI GAIRO



6
9
10
12 
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Kilosa wakimsikiliza Ndugu Abdurahman Kinana wakati alipokutana nao leo katika mkutano wa ndani mjini Kilosa
3
4
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana kulia akizungumza na Mohamed Seif Khatib katikati na Mjumbe wa Katibu wa NEC Idara ya Oganizesheni na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro  INNOCENT KALOGERIS mara baada ya kuwasili Wilayani Gairo wakitokea Wilayani Kilosa ambako kabla ya kuondoka kulifanyika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kilosa Town mjini Kilosa pia ilifanyika  mikutano ya ndani ambapo Katibu Mkuu aliongea na viongozi wa mashina, Madiwani wenyeviti, wajumbe na waasisi wa chama hicho ikiwani pamoja na kufungua mashina katika kuimarisha chama na kukagua baadhi ya shughuli za maendeleo, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi 6 
Kikundi cha  ngoma za asili ya kabila la Wapogolo kikicheza ngoma hiyo kabla ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kilosa Town na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali pamoja na wafuasi wa chama hicho
  5 

MASHINDANO YA NGUMI TEMEKE YAFANA INGAWA HAYANA WADHAMINI

masumbwiiiiiiiii
Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala
Na mwandishi wetu
MASHINDANO ya klabu  bingwa ya Mkoa wa Temeke yameanza jana jijini, Dar es Salaam huku yakishirikisha timu 20 na yanatarajiwa kufikia tamati  Aprili 19 mwaka huu.
 Lengo la mashindano hayo yaliyoanza jana ni kuinua vipaji vya mabondia chipukizi na kupata vipaji bora watakaokuwa chachu ya maendeleo ya mchezo nchini.
 Kocha wa kimataifa wa mchezo huo nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema vijana wanakaoshiriki mashindano hayo walipima uzito katika Ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke Dar es Salaam.
 Super D ambaye pia ni kocha wa timu ya Mkoa wa Ilala ambao ni waalikwa katika michuanohiyo alisema vijana wake kutoka klabu ya Amana na Ashanti watafanya vema katika mashindano hayo.
 Mkoa wangu umetoa vijana sita ambao naamini watafanya vizuri katika mashindano hayo kutoa upinzania mkubwa ambao utakuwa chachu ya maendeleo ya mchezo huo nchini.
Super D aliwataja baadhi ya mabondia hawo kuwa ni Hussein Mawimbi na Said Hamisi kutoka klabu ya Amana na Athumani Yanga pamoja na Said Mabunda kutoka klabu ya Ashanti.
 Pia aliwaomba wadau kujitokeza kusaidia mashindano hayo yanayofanyika katika ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke ili kuhakikisha hamasa ya kuendeleza mchezo huo inapatikana yatakayofanikisha mafanikio ambalo ndilo lengo kubwa. la mashindano hayo
 Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis  Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali

MZEE MWINYI AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati alipozungumzia swala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa kipindi cha hivi karibuni.
2

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BALOZI WA OMAN NCHINI


bk 2
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe Yahya bin Moussa al Bakari ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Mazungumzo hayo yalihusu mambo mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi mbili hizi.
bk 1

DKT BILALI AWATAKA VIONGOZI WA MAMLAKA ZA UDHIBITI NCHINI KUWA WAWAZI JUU YA KAZI ZA

Dr-Gharib-Bilal
Makamu wa Raisi Dkt Gharib Bilali amewataka viongozi pamoja na Mamlaka
za udhibiti hapa nchini kuhakikisha kuwa kabla hawajatoa maamuzi yao
wanawashirikisha wadau wao ikiwa ni pamoja na kuwa na tabia ya kuwa
wawazi ili kuweza kuboresha Mamlaka hizo.
Dkt Bilali aliyasema hayo mapema leo wakati akifungua mkutano wa
muungano wa mamlaka  za Miundo mbinu  barani Afrika (AFUM)
unaonendelea Jijini hapa.
Alisema kuwa kwa sasa kila mamlaka za usafirishaji zina takiwa
kuhakikisha zinajiwekea utaratibu wa kutotoa maaamuzi wanayotaka wao
wenyewe na badala yake wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanahusisha wadau
wote
Aliongeza kuwa endapo kama watakuwa na maamuzi yenye uwazi basi
yataweza kuharakisha maendeleo pamoja na wawekezaji hasa kwa nchi ya
Tanzania pamoja na barani afrika kwa ujumla hali ambayo nayo itaongeza
ufanisi kwenye mamlaka hizo za udhibiti.
“nawasisitiza kuwa uwazi na uwajibikaji ndio sehemu pekee ya kuwafanya
muwe na sifa nzuri lakini hata kukwepa lawama kwa wananchi lakini pia
ninyi kama ninyi mna nafasi kubwa sana ya kuhakikisha kuwa mnaongeza
ubora wa mamlaka zenu jamani “aliongeza Dkt Bilali
Awali dkt Bilali alimpongeza  waziri wa Nchi ofisi ya raisi Dkt Mark
Mwandosya kwa kutoa kitabu ambacho kinaoenesha na kufafanua juu ya
masuala mbalimbali yanayohusu masuala yanayohusu mamlaka za udhibiti
hapa nchini
Alisema kuwa Kitabu hicho ambacho kimeandaliwa na Waziri huyo
kinatakiwa kutoa elimu kwa wananchi pamoja na mamlaka hizo za udhibiti
kwa kuonesha changamoto pamoja na suluhu ambazo wakati mwingine
zinachangia sana maendeleo ya nchi
Awali Profesa Mwandosya alisema kuwa kitabu alichokiandaa ambacho
kinahusu masuala ya udhibiti wa Mamlaka pia kinaweza kutumika na watu
wote hasa  wananchi ambao wakati mwingine wanashindwa kujua na
kuzielewa kazi maalumu za mamlaka hizo ndani ya nchi husika
Mbali na hayo alisema kuwa Kitabu hicho pia kitaweza kuwafikia
wanafunzi hasa wale wa masomo ya biashara ambao wataweza kujifunza na
kisha kuona jinsi ambavyo wataweza kusaidia jamii zao

WABUNGE WASHAURIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA KUANZISHA BENKI ZA JAMII


WABUNGE
Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.
 SERIKALI inahakikisha kuwa inaweka mazingira bora na salama ya kiuchumi ili kuwezesha sekta binafsi kuanzisha mabenki na kutoa huduma bora za kibenki kwa wananchi.
 Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Kwela Mhe. Ignas Aloyce Malocha aliuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha akitaka kujua ni lini Serikali itashawishi taasisi za kifedha kuanzisha matawi yao katika mji mdogo wa Laela.
 Naibu Waziri Fedha Mhe. Saada Mkuya Salumu kwa niaba ya Waziri Fedha alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa wananchi kupata huduma za kibenki karibu na maeneo yao na pia serikali inatambua kuwa huduma hizo za kibenki kwa wananchi kazima ziwe zenye faida kwa pande zote mbili yaani kwa mabenki na wateja.
Naibu Waziri aliongeza kuwa kwa kuzingatia sera ya sasa ya huduma za mabenki, waheshimiwa Wabunge wanaweza kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wananchi kujiunga na kuanzisha benki za jamii (Community banks) zinazozingatia mazingira ya mahali husika pamoja na kuzihamasisha benki zilizopo nchini kufungua matawi katika maeneo hayo.
 “Serikali kwa kutambua umuhimu wa suala hili, imewasiliana na Benki ya NMB ambao wamekubali kwenda Laela kutathmini mazingira ya kibiashara kabla ya kufungua tawi mahali hapo”. Alisema Naibu Waziri huyo.
Akijibu maswali mawili ya nyongeza toka kwa mbunge huyo ambayo yalitaka kujua kwanini serikali isitumie Mobile Banking na kwanini benki hutoza riba kubwa, Mhe. Mkuya alijibu kwa kusema kuwa serikali haitumii mobile banking hivyo itashawishi benki nyingine zianzishe huduma hizo.
Kuhusiana na riba kubwa itozwayo na mabenki, Naibu Waziri alisema kuwa riba kubwa inategemea na benki zenyewe zinavyotumia gharama kubwa na riba katika kutoa huduma hivyo nao hawanabudi kupandisha riba kwa wateja wao.
Serikali kupitia Benki Kuu, imeweka sheria na taratibu za kusaidia juhudi za wananchi katika kuanzisha mabenki au taasisi za fedha katika maeneo yao. Serikali pia inayo sera ya Taifa inayolenga kuhamasisha uanzishwaji wa mabenki kwa ajili ya wateja wadogo (National Microfinance Policy) na sera hii inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments