LUIS SUAREZ KIFUNGO MECHI 10!!, BALAA LINGINE KWA MAJOGOO WA JIJI!!
Baraka Mpenja wa Fullshangwe kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji nyota wa Liverpool,
Luis Suarez, leo amepewa Adhabu ya Kufungiwa kutocheza Mechi 10 na FA,
Chama cha Soka England, kwa Kosa la kumng’ata meno Beki wa Chelsea,
Branislav Ivanovic, kwenye Mechi kati ya Liverpool na Chelsea
iliyochezwa Jumapili iliyopita.
Katika Mechi hiyo ambayo ilitoka
2-2, Refa Kevin Friend hakuliona tukio hilo lakini Ivanovic alilalamika
kwa Refa na kumuonyesha mkono wake ulioumwa.
Mara baada ya Mechi hiyo Suarez aliomba radhi na Klabu ya Liverpool ilimpiga Faini.
Baada ya FA kupata Ripoti ya Refa
Friend, ambae alikiri kutoliona tukio hilo, njia ikawa wazi kwa FA
kumfungulia Mashitaka Suarez ambae alikiri Kosa lakini aliomba Adhabu
yake ibakie Kifungo cha Mechi 3.
Ikitoa Adhabu hiyo, Jopo Huru la
FA lilikubali Kifungo cha kawaida cha Mechi 3 kwa Kosa la kuleta vurugu
na kuongeza Mechi nyingine 7 kwa kuzingatia uzito wa kosa lenyewe la
kinyama.
Adhabu hiyo inaanza mara moja
ikimaanisha Suarez atazikosa Mechi zote 4 Liverpool ilizobakisha kwa
Msimu huu pamoja na Mechi zao 6 za kwanza za Msimu mpya wa 2013/14
utakaoanza Mwezi Agosti.
Suarez amepewa hadi Ijumaa hii Saa 9 Mchana, Bongo Taimu, kukata Rufaa ikiwa hakuridhika na Adhabu.
Nimerudi: Luis Suarez akiwa mazoezini leo hii baada ya FC kumfungia mechi 10
Suarez akizamisha meno yake katika mkono wa beki wa Chelsea Branislav Ivanovic wakati wa mechi yao ya ligi kuu uwanjani Anfield.
Mwamuzi wa mchezo huo Kevin Friend akiambiwa na Ivanovic kwamba Suarez kaning`ata
Ivanovic akiwa amkeaa chini kuugulia maumizi ya kung`ata na Surezi.
VIFUNGO VIREFU TOKA FA:
-MIEZI 9: Mchezaji wa Manchester United Eric Cantona kwa kumpiga Mshabiki Mwaka 1995
-MIEZI 9: Kipa wa Chelsea Mark Bosnich kwa kugundulika kutumia Kokeni Mwaka 2003
-MIEZI 8: Rio Ferdinand wa Manchester United kwa kukosa kupimwa utumiaji Madawa yanayokatazwa hapo Mwaka 2003
-MECHI 12: Joey Barton wa QPR kwa kuleta vurugu kwenye Mechi na Man City Mwaka 2012.
-MECHI 11: Paolo Di Canio alipokuwa Sheffield Wednesday kwa kumsukuma Refa Paul Alcock Mwaka 1998
-MECHI 10: David Prutton wa Southampton kwa kumsukuma Refa Alan Wiley Mwaka 2005
-MECHI 10: Luis Suarez kwa kumuuma Branislav Ivanovic Mwaka 2013
-MECHI 9: Paul Davis wa Arsenal kwa kumpiga ngumi Glenn Cockerill wa Southampton Mwaka 1988 na kumvunja taya.
-MECHI 8: Luis Suarez kwa kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra Mwaka 2011
-MECHI 8: Ben Thatcher wa Man City kwa kumpiga kipepsi Pedro Mendes wa
Portsmouth Mwaka 2006.
-MECHI 5: Roy Keane wa Man United kwa kuandika maneno yasiyokubalika kwenye Kitabu chake hapo Mwaka 2002
JKT RUVU YAWAFUMUA LYON 1-0 CHAMAZI, MNYAMA VS RUVU SHOOTING KIMBEMBE KINGINE KESHO TAIFA!!
Baada
ya kufumuliwa mabao 3-0 na vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara Dar
Young Africas, leo hii maafande wa JKT Ruvu wamepunguza machungu baada
ya kuwatungua vibonde wa ligi hiyo Africa Lyon bao 1-0 mchezo uliopigwa
dimba la Chamazi jijini Dar es salaam.
Kocha
msaidizi wa JKT Ruvu Greyson Haule alisema wapinzani wao leo wamecheza
vizuri sana lakini bahati katika mchezo huo iliangukia upande wao.
“Hakika
mchezo ulikuwa mgumu, lakini kiwango cha timu yangu kinaniridhisha siku
hadi siku licha ya kuachwa na kocha wetu Charles Kilinda, lakini sasa
tunaye mwalimu Keny Mwaisabula ambaye kiukweli kachangia mambo mengi
sana” . Alisema Haule.
Haule
aliongeza kuwa kushinda mchezo wa leo ni hatua kubwa kwao kwani
wanajipa matumaini mazuri ya kufanya vizuri mechi zilizosalia.
Kocha
huyo alisema sasa hesabu zao ni mchezo ujao dhidi ya maafande wa
Tanzania Prisons “Wajelajela” ambao wanajiandaa kunyakua mzigo wa pointi
tatu muhimu.
“Tunajiandaa
kufanya vizuri na lazima shughuli iwe nzito na Prisons, tuna morali
kubwa na mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi kwasababu tuna uhakika wa
kubakia ligi kuu msimu huu”. Aliongeza Haule.
Baada
ya shughuli ya leo Taifa, hapo kesho kibarua kingine ni kati ya wekundu
wa Msimbazi Simba watakaowakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka
mkoani Pwani katika dimba la taifa.
Kuelekea
katika mchezo huo, kocha msaidizi wa klabu ya simba, Jamhuri Kiwhelo
Julio alisema wachezaji wote wapo salama na wanajiandaa kukumbana na
wanajeshi hao ambao wako sawa kwa kila idara”.
“Shooting
ni timu nzuri na kila mtu anajua, matokeo yoyote yatakayopatikana
tutamshukuru Mungu, wachezaji wanajua ugumu wa mechi lakini kocha Liwieg
kushirikiana na mimi tumefanya maandalizi kwa wachezaji wetu”. Alisema
Julio.
Julio
alisema kufungwa ni jambo la kawaida katika mchezo wa soka huku
akitolea kipigo cha jana walichokipata Barcelona kutoka kwa Bayern
Munich cha mabao 4-0.
“Jana
kila mtu alikuwa anashangaa, lakini soka ni mchezo wa mahesabu,
ukikosea unapigwa, na ndio maana jana Barca walicheza ovyo wakapigwa
kipigo cha mbwa mwizi, na sisi tukifungwa sio ajabu”. Alisema Julio.
Kocha
huyo aliwataka mashabiki wa simba kuwaombea dua njema wachezaji wao ili
waamke salama hapo kesho, lakini pia wajitokeze uwanjani kuwashangilia
vijana wao.
Kwa
upande wa Ruvu Shooting, afisa habari wa klabu hiyo Masau Bwire alisema
wamejiandaa kuwafunga simba wanaosikika wakisema wanataka kulinda
heshima mechi zilizosalia baada ya kupoteza ubingwa wao msimu huu..
“Tumesikia
maneno ya wana Simba kuwa wanataka kutufunga na kulinda heshima,
mwalimu Mkwasa mnamjua, kafanya mambo yake na kesho mnyama hatoki
kwetu”. Alijigamba Masau.
JENGENI TABIA YA KUPIMA UGONJWA WA KISUKARI- DK. MWINYI
Dk. Hussein Mwinyi
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
IMEELEZWA
kwamba inakadriwa kuwa asilimia saba ya idadi ya watu wazima wanaugua
ugonjwa wa kisukari, lakini chini ya 1/3 ndio wanaofahamu wana tatizo
hilo.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein
Mwinyi wakati akizindua kliniki ya vikoba ya wagonjwa wa kisukari
uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dares Salaam.
Dk.
Mwinyi alisema watu wanaokabiliwa na tatizo hilo, wanafika hospitalini
wakiwa wameathirika figo, macho, shinikizo la damu au kukatwa miguu.
“
Ninaishauri jamii kutumia huduma hiyo ili kuweza kuchunguza afya zao na
kujinga kwa kufuata kanuni za afya kama vile kula vyakula visivyo na
mafuta mengi, sukari nyingi, chumvi kiasi, kula mboga za majani kwa
wingi na matunda,” alisisitiza. Dk. Mwinyi.
Aliongeza pia jamii inatakiwa kufanya mazoezi ya kutosha, kupunguza
uzito kwa kiwango kinachotakiwa, kutovuta sigara na kupunguza kunywa
pombe au kuacha kabisa.
Dk.Mwinyi
alisema 1/3 ya idadi ya watu wazima wanakabiliwa na shinikizo la damu,
lakini chini ya asilimia 10 ndio wanafahamu kuwa wameathirika na tatizo
hilo.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania,
Dk.Kaushik Ramaiya alisema kliniki hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano wa
chama hicho na wizara hiyo ili kuboresha huduma za afya nchini.
Pia imetolewa na Novo Nordisk wakishikikiana na Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Duniani.
Alisema
kliniki hiyo ambayo itakuwa na inatoa tiba kwa wagonjwa wa
kisukari hususan watoto inafaa vifaa vya kisasa kwa ajili ya upimaji
wa matatizo ya kisukari ,macho,meno na mahabara ikiwemo genereta
itakatotumika sehemu ambazo hazina umeme . Pia itatoa huduma hiyo kwa
watu wazima .
Aliongeza kuwa kliniki hiyo ni ya kwanza kuzinduliwa ni maalum kwa
kanda ya ziwa ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi. Hivyo hapo
baadae watatoa nyingine kwa ajili ya kanda zingine.
Katika uzinduzi huo jumla ya watu wapatao 79 walijitokeza kupima afya zao na kupata ushauri mbalimbali.
0 Comments