Random Posts

MHE.RAIS NAWASILISHA KUTOKA KWA MKURUGENZI WANGU JUMA PINTO

SONY DSC
Mwandishi wa michezo na burudani wa Gazeti la Jambo Leo Bw.Magendela Hamisi akipewa mkono wa pongezi na Mhe.RAIS Jakaya Kikwete kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Jambo Concerpt. Juma Pinto.kwa mchango wake alioutoa kwenye harambee ya kutunisha mfuko wa kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wananchi wanaoishi Jimbo la Ukonga kuwainua kimaendeleo .ulifanyika hivi karibuni kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es es salaam.
(PICHA ZOTE NA PHILEOMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

RED COAST, ABAJALO, FRIENDS RANGERS ZAFUZU HATUA YA KANDA!!

a
Red Coast, Abajalo, Friends Rangers zafuzu hatua ya Kanda
Ligi Daraja la Pili mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora imemalizika leo kwa timu tatu za Red Coast,  Abajalo na Friends Rangers zimefuzu kucheza hatua ya Kanda.
Katika mechi iliyochezwa Makurumla, Friends Rangers iliifunga Sharif Stars mabao 2-0. Mabao hayo yamefungwa na Khatib Kuduku katika dakika ya 12 na Mwenda Athuman katika dakika ya 57.Kwa matokeo hayo Rangers imefikisha pointi 8.
Kwenye uwanja wa Kinesi Red Coast wameibuka na  ushindi wa bao 1-0.Bao hilo limefungwa dakika ya 32 na Rafael Mapunda. Kwa matokeo hayo Red Coast wamefuzu hatua hiyo kwa kujikusanyia pointi 11 wakiwa vinara wa ligi hiyo.
Abajalo nao wamefuzu hatua hiyo baada ya kuichapacha Boom FC mabao 2-0. Hata hivyo mechi hiyo ilivunjika kutokana na wachezaji watatu wa Boom FC kutolewa kwa kadi nyekundu.Abajalo imeweza kufuzu baada ya kujikusanyia pointi 10.

HUU NDIYO UTAMU WA KUPORA

SONY DSC 

Kibaka ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akiwa chini ya ulinzi wa raia wenye hasira kali baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi hao akituhumiwa kumpora simu mpita njia eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam jana.

TUNAJADILI RASIMU YA KATIBA YA SOKO LA KIBASILA

SONY DSCMwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara soko la Kibasila (UWASOKI)kushoto Bw.Juma Liahumako.akitoa ufafanuzi wakati akifungua mkutano wa kujadili rasimu ya katiba soko la kibasila lililoko Manispaa ya ilala uliofanyika leo katika ukumbi wa shule ya msingi Uhuru  jijini Dar es salaam.moja ya rasimu hizo zlizokuwa zikijadiliwa ni kuwashirikisha wafanyabiashara wa soko hilo kutoa huduma bora kwa wateja na kudumisha umoja undugu miongoni mwa wafanyabiashara .kufanya shughuli zote halali kulingana na sheria za nchi.(katikati)Makamu mwenyekiti wa soko hilo Bw.Nasibu Ibwe.(kulia)Afisa afya kata ya gerezani Bi.Safihuma Mdee. SONY DSCMwanachama wa soko la kibasila Bw.Issa Namchuku.akichangia mada wakati wa mkutano wa kujadili Rasimu ya katiba soko la kibasila. (PICHA ZOTE NA PHILEOMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA TZ METHODIST MSASANI NA KUZINDUA CD YA KWAYA YA WATOTO WANAOFADHILIWA NA COMPASSION INTERNATIONAL TZ

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya maua kutoka kwa watoto wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Joseph Mayala, leo  wakati wa hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo. Kulia ni Askofu wa Kanisa hilo, Dkt. Mathew Byamungu. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristo wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
 Baadhi ya waumini waliohudhuria harambee hiyo.
 Watoto wa Kwaya inayofadhiliwa na Shirika la Compassion International Tanzania, wakitoa burudani ya kuimba moja ya wimbo wao ulio katika Albam yao iliyozinduliwa katika hafla hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Watoto wa Kituo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wachungaji na watumishi wa Kanisa hilo.

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA KILELE CHA MIAKA 10 YA FAO LA ELIMU LINALOTOLEWA NA PPF.

IMG_9901 
Naibu Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Kmuya Salum akimkabidhi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete zawadi wakati wa sharehe ya kutimiza miaka 10  ya Fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF zilizofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar tarehe 27.4.2013
. IMG_9626 
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaofadhiliwa na PPF katika masomo yao wakiwa kwenye sherehe ya kutimiza miaka 10 ya Fao la Elimu litolewalo na shirika hilo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convetion Centre jijini Dar tarehe 27.4.2013. IMG_9670 
 Binti mcheza sarakasi kutoka katika kikundi cha Safi akionyesha umahili wa michezo mbalimbali kama anavyoonekana kaytika picha hiyo. IMG_9697 
Baadhi wa wazazi na wanafunzi  waliopata fursa ya huduma ya elimu kutoka katika mfuko wa PPF wakipiga picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya kutoa ushuhuda wao wa jinsi gani mfuko huo umeweza kuwasaidia.
Kundi la muziki wa Taaiab likitumbuiza katika hafla hiyo. IMG_9712 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwatuza waimbaji wa taarabu wakati wa sherehe ya miaka 10 ya Fao la elimu linalotolewa na PPF iliyofanyika Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar tarehe 27.4.2013. IMG_9716 
Naibu Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya Salum akimpongeza Bi Asha Mashauzi wakati wa sharehe ya miaka 10 ya Fao la elimu linalotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF. IMG_9717 
Wageni waalikwa pamoja na wanafunzi waliOshiriki katika sherehe za kutimiza miaka 10 ya Fao la elimu linalotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar tarehe 27.4.2017. IMG_9806 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wakati wa kilele cha kutimiza miaka 10 ya Fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre hapa Dar tarehe 27.4,2013. IMG_9807 
Wageni waalikwa pamoja na wanafunzi waliOshiriki katika sherehe za kutimiza miaka 10 ya Fao la elimu linalotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar tarehe 27.4.2017.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na kupata division 1 na 2 katika masomo yao. Wanafunzi hao walitunukiwa compyuta ya kisasa kila mmoja. IMG_9873 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na kupata division 1 na 2 katika masomo yao. Wanafunzi hao walitunukiwa compyuta ya kisasa kila mmoja. IMG_9890 
Baadhi ya wanafunzi  waliopata fursa ya huduma ya elimu kutoka katika mfuko wa PPF wawa na kompyuta zaomara baada ya kuzawadiwa na mgeni rasmi 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa mkono mwanafunzi mdogo wa shule ya msingi mara baada ya sherehe ya kutimiza miaka 10 ya Fao la elimu linalotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF zilizofanyika jijini Dar tarehe 27.4,2013.
IMG_9996 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya udhamini na wanafunzi wanaofadhiliwa katika elimu yao na PPF wakati wa kilele cha kutimiza miaka 10 zilizofanyika Dar tarehe 27.4.2013.

Post a Comment

0 Comments