NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia Januari Makamba amesema dhamira ya kuwepo kwa vyama vingi bado
haijafikiwa tangu kuanzishwa kwake kutokana na kukosa vyama na viongozi
wenye dira kwa Taifa.
Aliyasema hayo leo jijini Dar es
Salaam wakati akizungumza na wamnafunzi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambao
wanamaliza vyuo mbalimbali mkoa wa Dar es Salaam.
Makamba ambaye pia ni Mlezi wa Vyuo
Vikuu Tanzania alisema vyama hivyo vimekuwa vikijikita katika kulalamika
bila kuonyesha dira na mwelekeo tofauti jambo ambalo linapelekea katika kufanya
fujo ambazo zinakwamisha jitihada za serikali.
Makamba alisema Serikali inafanya
kazi kutokana na mipango yake ambayo imejiwekea yenyewe hivyo inaamini kuwa
itafikia malengo yake bila kusukumwa na mtu.
“Kwa kweli najuta kwanini
tuliruhusu uwepo wa vyama vingi hapa nchini kwani lengo letu lilikuwa ni
kudumisha demokrasia kitu ambacho kimekuwa kinyume kwani vyama na
viongozi hao wamekuwa wakihubiri kinyume na dhima ya lengo husika,” alisema
Naibu Waziri alisema CCM ni chama
ambacho kinaheshimika kitaifa na kimataifa hivyo wao wanaamini kuwa heshima
hiyo itaendelea kuwepo milele kwa milele.
Alisema vijana wa CCM wahakikishe
kuwa wanakisaidia chama na nchi kwa ujumla ili nchi isije kuchukuliwa na
vyama vya upinzani kwani itakuwa ni sawa na kuipeleka nchi kuzimu.
Aidha Mlezi huyo aliwataka vijana
hao wanaomaliza kujiamini na kuthubutu kushiriki katika fursa mbalimbali
zinazojitokeza ili waweze kupata urahisi wa kushiriki katika chama na serikali
kwani ni wajibu wao kulitumikia Taifa.
Makamba alisema vijana wanapaswa
kushiriki katika harakati za kisiasa kwani hayupo mtu amnbaye atapata jambo
bila kulihitaji mwenyewe na kuondokana na dhana ya kutafutiwa kazi kama wengi
wanaofikiri.
Aliwataka wingi wao uwe ni sehemu
muhimu ya kutafakari muafaka wa Taifa la Tanzania ijao ikiwa ni kushiriki
katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuondokana na dhana kuwa mwenye uwezo wa
fedha ndio sababu ya kushinda.
Mlezi huyo alisema dhana ya fedha
katika kutafuta uongozi ipo kwa baadhi ya watu kutokana na tabia ya mtu
mmoja mmoja lakini sio jambo la kusimamia kama kigezo.
Naibu Waziri aliwataka vijana wa CCM
kuondoa uoga katika maamuzi ambayo yanahusu maslahi ya Taifa na jamii kwa
ujumla iwapo sifa za uongozi unazo.
Makamba aliwaambia vijana kutambua
kuwa kiongozi wema wanatoka kwa mungu na kuachana na tabia ya kulalamika
kwakigezo kuwa nchi inaongozwa na wazee jambo ambalo wanalitengeneza wenyewe.
Aidha aliwataka wasomi kutafuta
maandiko ambayo aliandika Hayati Mwalimu Nyerere kwani yana msingi mkubwa
katika kujitambua na kufanya maamuzi sahihi kuhusu nchi yao na uongozi kwa
ujumla.
Naye Mwenyekiti Vyuo Vikuu
Wilaya ya Dar es Salaam Abubakari Asenga alisema katika mahafal;i hayo
wanafunzi zaidi ya mmia nne kutoka vyuo 28 vya mkoa wa Dar es Salaam
walishiriki katika sherehe hiyo.
Asenga alisema huo ni uataratibu
ambao wamekuwa nao tangu kuoanzishwa kwa shirikisho hilo lengo likiwa ni
kuwatambua na kuwapatia vyeti vya utambulisho wao ndani ya CCM.
Alitaja vyuo ambavyo vilishiriki ni
pamoja na Mwalimu Nyerere, Ustawi, Ardhi, UDSM, IFM, CBE, DIT, TSJ na vingine
vingi.
Kwa upande wa msoma risala kwa niaba
ya wahitimu Innocent Nsena alisema wanakiomba Chama Cha Mapinduzi CCM
kuwatumia wahitimu wanaomaliza vyuo kwani wana ujuzi na uwezo wa kukabiliana
na changamoto za jamii pamoja na vyama vya upinzani hapa nchini.
Aidha alisema wanavyuo wanapendekeza
maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ambapo wanaomba nchi ya Tanzania kutokubali
kuwa na serikali ya shirikisho kwani uwezo wa nchi bado ni mdogo kuendesha nchi
ambayo bado ni change kuichumi.
Pia wanapendekeza upatikanaji mpya
wa kupata mgombea urais ili kuondoa mpasuko ambao unatokea mara kwa mara baada
ya uchaguzi kufanyika.
Alisema katika mazingira yoyote yale
Rais bora lazima atokee CCM ila kutokana na mazingira mbalimbali ambayo
yamekuwa yakitokea baada ya uchaguzi ni vyema wakatumia mfumo wa kujaza dodoso
ili wana CCM wapendekeze Rais wanayemuhitaji kwa manufaa ya Taifa.

0 Comments