Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini, Washington, DC, Marekani na
Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia
wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha ni
kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto
wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake
kizazi hadi kizazi.
Siku ya July 6, 2013 hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo
207 w Hampton Pl,
Capitol Height, MD
Mambo
mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, Asya Idarous
mwanamitindo ya mavazi kutoka Tanzania akishirikiana na hapa Marekani,
vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekani yote ni
kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili
TEGA SIKIO, HABARI ZAIDI ZITAFUATA
——————————————————-
kwa
wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya
kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613
5165, 301 661 6696 na 301 792 8562 mwisho ni June 15, 2013 Asante
NO COVER CHARGE, FREE DINNER

0 Comments