Katika
salaam zake za pongezi Kamishna Jenerali Minja pia amewapongeza Wakuu
wa Magereza Mikoa, Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, na Askari wote
kwa jumla kwa namna walivyoweza kushiriki kikamilifu katika kuleta
ushindi wa kwanza katika Taasisi za Uzalishaji za Serikali, Banda Bora,
Kilimo na Mifugo hata katika Maonesho ya Kikanda ikiwemo Kanda ya
Magharibi iliyojumuisha Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora pamoja na
Kanda ya Mashariki iliyojumuisha Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na
Morogoro kwa kuibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za
Uzalishaji za Serikali.
“Nimepokea
kwa furaha kubwa na shangwe habari za ushindi huo wa kwanza wa jumla
katika Maonesho ya Wakulima Kitaifa na hata ushindi wa kwanza kwa upande
wa Taasisi za Uzalishaji za Serikali katika Baadhi ya Kanda ambazo
Jeshi la Magereza limeshiriki”.
Kwa
niaba ya Serikali na kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kuwatumia salaam
hizo za pongezi kwa ushindi huo kwani matokeo haya siyo yamenyesha tu
kama mvua ya ghafla, bali ni matokeo makubwa ya mpango mkakati
tuliouasisi – ninyi na mimi tangu nilipoteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kuapishwa rasmi
tarehe 25 Septemba, 2012 kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini.
Aidha,
amesisitiza kuwa ushindi huo bado ni changamoto kwa Jeshi la Magereza
kuhakikisha kuwa wanajipanga vyema katika Maonesho mengine yanayofuata
ili kuendelea kutetea nafasi hiyo ambayo imeleta sifa kubwa kwa Jeshi la
Magereza hivyo kutekeleza mpango kazi wa sasa katika utendaji wa kazi
unaotaka Matokeo makubwa sasa(Big Results Now).
Maonesho
hayo ya Wakulima hufanyika kila Mwaka Kitaifa na Kikanda ambapo Kitaifa
katika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma jumla ya washiriki zaidi ya 400 kutoka
Wizara, Idara, Taasisi za Serikali zinazojitegemea na Makampuni Binafsi
wameshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo ambayo yamefungwa jana na
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Seif Idd.
Imetolewa na Mkaguzi wa Magereza, Lucas Mboje,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza Nchini.
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza Nchini.
0 Comments