Random Posts

TATIZO LA WATOTO MITAANI LAZIDI KUSHIKA KASI JIJINI DAR ES SALAAM

Baadhi ya watoto ombaomba wakiwa wamelala kama walivyo kutwa na mpiga picha wetu eneo la kisutu jijini Dar es salaam leo huku tatizo la watoto wa mitaani likizidi kushika kasi kila kukicha 

PICHA NA BERNARD JAMES WA MTAZAMO MEDIA DAR ES SALAAM


Na Bernard James wa Mtazamo Media Dar es salaam



Watoto wadogo wanao tumiwa na wazazi wao kuomba katika mitaa mbalimbali jijini Dar es salaam  limezidi kuongezeka na kushika kasi kila kukicha huku vyombo husika vikiwa kimya kama vile hakuna tatizo.MTAZAMO limegundua upashanaji habari zakuitana kuja jijini kwa wazazi wanaowatumia watoto wao wadogo kuomba na wale ambao wako mikoani hasa mkoa wa Dodoma kuja jijini Dar Es Salaam na kwamba hakuna usumbufu,akiongea kwa masikito  MR Munis ambae ni Dalali katika soko la Ndizi Mabibo ameshangazwa na Wizara husika kutochua hatua kwa kuwakata na kuwarudisha makwao wazazi wanao watumia watoto kuomba omba ,huku wakionekana wanao uwezo wakufanya kazi,angalia hali ilivyo je?hawa watoto wanakosa haki yao ya msingi ya kupata Elimu,alisema Munis

Post a Comment

0 Comments