![]() |
| Rais Dr Jakaya Kikwete |
![]() |
| Viongozi wa UKAWA |
Askofu Dr Boaz Sollo akiwa katika moja kati ya mikutano yake ya kuliombea Taifa amani
Na Francis Godwin Blog
UMOJA wa katiba ya wananchi
(UKAWA) wazidi kukaliwa kooni baada ya askofu wa kanisa la
Overcomers Power Centre Iringa Dr Boaz Sollo kupinga vikali uamuzi wa
UKAWA kutoka bungeni na kwenda kwa wananchi kabla ya kuifanya kazi
waliyotumwa bungeni kama wajumbe wa bunge la katiba na hivyo
kumshauri Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete
kulivunja bunge hilo ili kuepusha amani kuvurugwa nchini.
Huku
akisema kuwa akiwa kama mtumishi wa Mungu anaamini kabisa kuwa
serikali mbili ni jibu la watanzania katika endeleza umoja ,amani na
mshikamano ulioachwa na waasisi wa Taifa hili hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Raiswa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuvurungwa na wanasiasa wachache wasiopenda amani ya nchi hii .
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kwa
njia ya simu kutoka jijini Dar es salaam ambako amealikwa kwa huduma
za kanisa , askofu Dr Solloa alisema kuwa tayari kanisa lake
limeanza kufunga na kuomba kwa ajili ya amani nchini na kuliombea
bunge hilo la katiba ili mwenyezi Mungu kuliunganisha bunge hilo
na kuepusha mgawanyiko ulioanza kujitokeza na kundi hilo la wana
Siasa wanaojiita wana UKAWA .
”
Watamzania tulipongeza uteuzi wa Rais wetu mpendwa Dr Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kuteua miongoni mwa watanzania wachache kati ya wengi
kwa ajili ya kwenda kushiriki bunge hilo kuandaa katiba ya nchi huku
tukiamini kuwa walioteuliwa wangetufikisha pazuri zaidi tofauti na
ilivyo sasa ambapo wajumbe hao wameanza kuhatarisha amani na utulivu
nchini “
Kitendo
cha wajumbe wa bunge hilo kutoka nje ya ukumbi na kutaka kuanza
kuzunguka mikoani ni sawa na kuwasaliti wananchi ambao walikuwa
wakisubiri kwa hamu wajumbe hao kuwaletea katiba mpya ila sasa wameanza
kutishia amani ya nchi kwa kutafuta huruma ya wananchi katika kuungwa
mkono wao na vyama vyao.
”
Ushauri wangu kwa mheshimiwa Rais Dr Kikwete ni kulivunja kabisa
bunge hilo ili kunusuru amani ya nchi hii ambavyo dalili ya
kuvurugwa imeanza kujitokeza kupitia UKAWA ….tulitegemea wajumbe hao
wangebaki ndani ya bunge na kutuandalia katiba bila kuunda umoja wa
kuanzisha vurugu nchini kwani wote bila kujali vyama vyao na taasisi
zao walizotoka walipaswa kuwa kitu kimoja katika bunge hilo kwa
kuwasilisha hoja za kuwa na katiba bora si vinginevyo “
Alisema
kuwa ni vema kuendelea na katiba iliyopo kuliko kusubiri katiba ya
wajumbe hao ambayo mwelekeo wake si mzuri bali upo kwa ajili ya
matakwa ya wachache kisiasa .
Askofu
huyo alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wanachanganywa na wana siasa
hao ila ukweli wazanzibar na watanzania wanapenda kuona amani
iliyopo inaendelea kuwepo na suala la maendeleo linaendelea na sio
utitiri wa serikali hali maisha yao kiuchumi ni duni .
Hata
hivyo alisema kutokana na mwenendo wa bunge hilo kwa sasa kanisa
lake limetangaza mfungo wa maombi maalum kwa ajili ya Tanzania ili
kuepuka chuki kupandikizwa na wachache kwa lengo la kuvuruga amani yetu
.

